Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Baada ya ndugu katika makao makuu kusoma ripoti ya John kuhusu ziara yake nchini Albania, walimweka Leonidha Pope, Sotir Papa, na Luçi Xheka kusimamia Kutaniko la Tiranë na vilevile kazi nchini Albania.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Muda si muda, ripoti zikaanza kuonyesha kwamba ndugu hao wameelewa vizuri maagizo waliyopewa. Ndugu watatu waliokuwa Tiranë walitenda wakiwa Halmashauri ya Nchi, naye Spiro alikuwa akiyatembelea makutaniko kwa ukawaida.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MWANZO MZURI—KISHA MATATIZO

      Ingawa Halmashauri ya Nchi ilijitahidi kuendeleza ibada safi, matatizo yalikuwa njiani. Mwaka wa 1963, Melpo Marks alimwandikia John, ndugu yake, kwamba ndugu wawili wa Halmashauri ya Nchi, Leonidha Pope na Luçi Xheka, hawakuwa “pamoja na familia zao” na kwamba mikutano haifanywi. Baadaye kukawa na fununu kwamba Spiro Vruho yuko hospitalini, naye Leonidha Pope na Luçi Xheka ni wagonjwa, andiko la Matendo 8:1, 3 lilirejelewa, ambapo Sauli wa Tarso aliwatia Wakristo gerezani. Ni nini kilichokuwa kikiendelea?

      Leonidha Pope, Luçi Xheka, na Sotir Ceqi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda fulani ambapo washiriki wa Chama cha Kikomunisti walifanya mkutano na wafanyakazi wote, wakipigia debe dhana za Kikomunisti. Siku moja, kulipokuwa na mazungumzo kuhusu mageuzi, Leonidha na Luçi walisimama na kusema: “Hapana! Mwanadamu hakutokana na nyani!” Siku iliyofuata walichukuliwa na kutenganishwa na familia zao, na kupelekwa kufanya kazi uhamishoni katika miji ya mbali, adhabu ambayo huitwa internim (korokoroni) na Waalbania. Luçi alipelekwa katika milima ya Gramsh. Kwa kuwa waliamini kwamba Leonidha ndiye “mkubwa” wao, walimpeleka katika milima ya Burrel, yenye mawe-mawe na baridi kali. Miaka saba ilipita kabla ya kurudi nyumbani kwao, Tiranë.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Akina ndugu waliokuwa wakiongoza hawakuwako. Nao waliobaki hawakuweza kuwasiliana kwa sababu ya upelelezi wa Sigurimi. Hata hivyo, ndugu waliokuwa korokoroni waliwatolea ushahidi mzuri mtu yeyote waliyekutana naye. Watu wa Gramsh walikuwa wakisema: “Ungjillorë [wainjilisti] wako hapa. Hawajiungi na jeshi, lakini wanatujengea madaraja na kurekebisha majenereta.” Sifa nzuri ya ndugu hao ilijulikana kwa miaka mingi.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mapema miaka ya 1960, Luçi aliwekwa kuwa mshiriki wa Halmashauri ya Nchi, iliyokuwa imeundwa ili kusimamia kazi nchini Albania. Muda si muda akahukumiwa kifungo cha miaka mitano huko Gramsh, mbali na Frosina na watoto wake. Akiwa huko, Luçi aliendelea kuhubiri na kuzungumza kuhusu tengenezo la Yehova. Watu wa Gramsh wanamkumbuka hadi leo hii.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki