Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Sokrat na Thanas Duli (Athan Doulis) walizaliwa nchini Albania, hata hivyo walihamia Uturuki wakiwa wangali wadogo. Sokrat alirudi Albania mwaka wa 1922. Mwaka uliofuata, Thanas pia, mwenye umri wa miaka 14, akarudi kumtafuta ndugu yake. “Nilipofika nyumbani,” akaandika, “sikumpata ndugu yangu. Alikuwa akifanya kazi zaidi ya kilomita 200 kutoka nyumbani. Hata hivyo, nilipata magazeti ya Mnara wa Mlinzi, Biblia, na mabuku saba ya Studies in the Scriptures, pamoja na vijitabu vingine vya Biblia. Inaonekana kwamba hata katika eneo hilo la mbali lenye milima-milima, kulikuwa na Wanafunzi wa Biblia wenye bidii waliokuwa wameishi Marekani ambao walirudi wakiwa na kiasi fulani cha ujuzi wa Biblia nao waliupenda ujumbe wake.” Ndugu hao wawili walipokutana hatimaye, Sokrat—aliyekuwa tayari amebatizwa—hakusita kumfundisha ndugu yake, Thanas, ukweli.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • “Mwaka wa 1925, kulikuwa na makutaniko matatu nchini Albania, na Wanafunzi wa Biblia waliokuwa mbali,” akaandika Thanas. Pia, anataja kwamba walikuwa na upendo mwingi tofauti kabisa na watu wengine waliokuwa na mizozo, kiburi, na roho ya mashindano.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki