-
Mtu Anapotaka Kuendelea KunywaMnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
-
-
Mtu Anapotaka Kuendelea Kunywa
ALLEN alianza kunywa pombe kupita kiasi alipokuwa na miaka 11.a Yeye na marafiki wake walicheza msituni wakiigiza watu mashuhuri waliokuwa wamewaona katika sinema. Watu waliowaigiza hawakuwa watu halisi, lakini bila shaka pombe ambayo Allen na marafiki wake walikunywa ilikuwa halisi.
Tony alikuwa na miaka 40 alipoanza hatua kwa hatua kuongeza kiasi cha pombe alichokuwa akinywa kila jioni. Hatimaye, hakujua kiasi cha pombe alichokuwa akinywa kila siku.
Allen aliomba msaada wa kuacha kunywa pombe kupita kiasi. Tony naye alikataa msaada wa watu wa familia yake na marafiki wake. Allen angali yuko hai leo; Tony alikufa miaka kadhaa iliyopita katika msiba wa barabarani uliotokea kwa sababu alikuwa amelewa.
-
-
Maoni ya Mungu Kuhusu PombeMnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
-
-
Allen aliyekuwa akinywa pombe kupita kiasi, ambaye anatajwa katika makala ya kwanza, anasema hivi: “Ulevi sugu si kasoro ya mwili tu; bali pia ni kasoro ya maoni na mtazamo wa mtu. Hajali jinsi anavyowaumiza watu wengine.”
-