-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
12. Ile “pembe kubwa” ya beberu wa mfano ‘ilivunjwaje,’ nazo zile pembe nne zilizotokea mahali pake zilikuwa nini?
12 Lakini nguvu ya Aleksanda ilikuwa ya muda mfupi tu. Lile ono laendelea kufunua hivi: “Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.” (Danieli 8:8) Gabrieli asema hivi akiufafanua unabii huo: “Katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.” (Danieli 8:22) Kama ilivyotabiriwa, kwenye upeo wa ushindi wake mbalimbali, Aleksanda ‘alivunjika,’ au akafa, akiwa na umri wa miaka 32 tu. Nayo milki yake kubwa hatimaye ikagawanywa miongoni mwa wanne kati ya majenerali wake.
-
-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
16. (a) Ile pembe ndogo ilitokana na pembe gani ya mfano? (b) Roma ilipataje kuwa serikali ya ulimwengu ya sita ya unabii wa Biblia, lakini kwa nini haikuwa ile pembe ndogo ya mfano?
16 Kulingana na historia, ile pembe ndogo ilitokana na mojawapo ya zile pembe nne za mfano—ile pembe iliyokuwa mbali zaidi upande wa magharibi. Hiyo ilikuwa ufalme wa Kigiriki wa Jenerali Kasanda aliyetawala Makedonia na Ugiriki. Baadaye, ufalme huo ulitwaliwa na Jenerali Lisimako, mfalme wa Thrasi na Asia Ndogo. Katika karne ya pili kabla ya Wakati wetu wa Kawaida, maeneo hayo ya magharibi ya utawala wa Kigiriki yalishindwa na Roma. Na kufikia mwaka wa 30 K.W.K., milki ya Roma ilitwaa falme zote za Kigiriki, na hivyo kuwa serikali ya ulimwengu ya sita ya unabii wa Biblia.
-