Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wayahudi Waathiriwa Na Utawala Wa Wagiriki Na Waroma
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • Milki ya Ugiriki

      UPANUZI wa Milki ya Ugiriki ulianzia milima ya Makedonia. Akiwa huko, Aleksanda mwenye umri wa miaka 20 hivi alianza kufikiria jinsi atakavyoteka maeneo yaliyokuwa upande wa mashariki. Katika mwaka wa 334 K.W.K., aliongoza jeshi lake kuvuka eneo la Hellespont (Dardanelles), linalotenganisha Ulaya na Asia. Likiwa kama “chui” mwenye mbio, jeshi la Ugiriki chini ya Aleksanda lilianza kuteka maeneo mengi haraka. (Da 7:6) Aleksanda aliwashinda Waajemi karibu na jiji la Troyi, kwenye nchi tambarare za Mto Granicus, kisha akawashinda kabisa huko Iso.

      Wagiriki walishambulia Siria na Foinike, na kuliharibu jiji la Tiro baada ya kulizingira kwa miezi saba. (Eze 26:4, 12) Aleksanda aliteka Gaza lakini hakushambulia Yerusalemu. (Zek 9:5) Alipofika Misri, alijenga jiji la Aleksandria ambalo hatimaye lilikuwa kituo cha biashara na elimu. Baada ya kuvuka tena Nchi ya Ahadi, aliwashinda kabisa Waajemi tena huko Gaugamela, karibu na magofu ya jiji la Ninawi.

      Aleksanda alielekea upande wa kusini na kuteka Babiloni, Shushani (Susa), na Persepoli—vituo vya kuendesha shughuli za serikali ya Uajemi. Kisha aliteka haraka maeneo ya Uajemi, na kufika Mto Indus, eneo ambalo ni Pakistan ya sasa. Kwa muda wa miaka minane tu, Aleksanda aliteka maeneo mengi yaliyojulikana wakati huo. Lakini katika mwaka wa 323 K.W.K., akiwa na umri wa miaka 32, Aleksanda aliugua malaria na kufa huko Babiloni.—Da 8:8.

  • Wayahudi Waathiriwa Na Utawala Wa Wagiriki Na Waroma
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • Njia ya Aleksanda

      A2 ▪ MAKEDONIA

      A2 ▪ Pella

      A2 ▫ THRACE

      B2 ▫ Troy

      B2 ▫ Sardi

      B2 ▫ Efeso

      B2 ▫ Gordium

      C2 ▫ Ankara

      C3 • Tarso

      C3 • Iso

      C3 • Antiokia (ya Siria)

      C3 ○ Tiro

      C4 ○ Gaza

      B4 ○ MISRI

      B4 ○ Memfisi

      B4 ○ Aleksandria

      A4 ○ Chemchemi cha Siwa

      B4 ○ Memfisi

      C4 ○ Gaza

      C3 ○ Tiro

      C3 ○ Damasko

      C3 • Aleppo

      D3 • Nisibis

      D3 • Gaugamela

      D3 • Babiloni

      E3 • Shushani

      E4 • UAJEMI

      E4 • Persepoli

      E4 • Pasargadae

      E3 • UMEDI

      E3 • Ekibatana

      E3 • Rhagae

      E3 • Hekatompylo

      F3 • PARITHIA

      G3 • ARIA

      G3 • Aleksandria Areioni

      G3 • Aleksandria Prophthasia

      F4 • DRANGIANA

      G4 • ARIACHOSIA

      G4 • Aleksandria Ariachosiorum

      H3 • Kabul

      G3 • Drapsaca

      H3 • Aleksandria Oxiana

      G3 • Drapsaca

      G3 • BACTRIA

      G3 • Bactra

      G2 • Derbent

      G2 • SOGDIANA

      G2 • Maracanda

      G2 • Bukhara

      G2 • Marakanda

      H2 • Aleksandria Eschate

      G2 • Marakanda

      G2 • Derbent

      G3 • Baktra

      G3 • BAKTRIA

      G3 • Drapsaka

      H3 • Kabul

      H3 • Taxila

      H5 • INDIA

      H4 • Aleksandria

      G4 • GEDROSIA

      F4 • Pura

      E4 • UAJEMI

      F4 • Aleksandria

      F4 • CARIMANIA

      E4 • Pasargadae

      E4 • Persepoli

      E3 • Shushani

      D3 • Babiloni

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki