Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu cha Danieli Chashtakiwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • USHUHUDA WA NJE UNAOTETEA DANIELI

      25. (a) Yosefo alithibitishaje ukweli wa simulizi la Danieli? (b) Simulizi la Yosefo juu ya Aleksanda Mkuu na kitabu cha Danieli lapatanaje na historia inayojulikana? (Ona kielezi-chini cha pili.) (c) Uthibitisho wa lugha wategemezaje kitabu cha Danieli? (Ona ukurasa wa 26.)

      25 Acheni tufikirie tena utetezi. Imedokezwa kwamba hakuna kitabu kingine cha Maandiko ya Kiebrania ambacho kimethibitishwa kuwa cha kweli kama kitabu cha Danieli. Kwa kielelezo: Yule mwanahistoria Myahudi ajulikanaye sana, Yosefo, athibitisha kwamba ni chenye kutumainika. Asema kwamba Aleksanda Mkuu alikuja Yerusalemu wakati wa vita yake dhidi ya Uajemi katika karne ya nne K.W.K., na huko makuhani walimwonyesha nakala ya kitabu cha Danieli. Aleksanda mwenyewe alikata kauli kwamba maneno aliyoonyeshwa ya unabii wa Danieli, yalirejezea kampeni yake mwenyewe ya kijeshi iliyohusisha Uajemi.e Hilo lingekuwa karne moja na nusu hivi kabla ya ule “udanganyifu” udaiwao na wachambuzi. Bila shaka, wachambuzi wamemshambulia Yosefo juu ya maneno hayo. Pia wamemshambulia kwa kutaarifu kwamba baadhi ya unabii wa kitabu cha Danieli ulitimizwa. Hata hivyo, kama vile mwanahistoria Joseph D. Wilson alivyosema, “Yamkini, [Yosefo] alijua mengi zaidi juu ya suala hilo kuliko wachambuzi wote duniani.”

  • Kitabu cha Danieli Chashtakiwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • e Wanahistoria fulani wametaarifu kwamba hilo lingeelewesha sababu iliyomfanya Aleksanda awe mwenye fadhili sana kwa Wayahudi, ambao walikuwa marafiki wa muda mrefu wa Waajemi. Wakati huo, Aleksanda alikuwa akifanya kampeni ya kuharibu marafiki wote wa Waajemi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki