Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ni Nani Atakayeutawala Ulimwengu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • Akiwa na umri wa miaka 13, Aleksanda alifundishwa na Aristotle, mwanafalsafa Mgiriki, ambaye alimsaidia kukuza upendezi katika falsafa, tiba, na sayansi. Watu wana maoni tofauti juu ya kiwango ambacho mafundisho ya Aristotle ya falsafa yaliathiri njia ya kufikiri ya Aleksanda. “Yaelekea kuwa sahihi kusema kwamba kuna mambo mengi ambayo watu hao wawili hawakukubaliana,” akaonelea Bertrand Russell, mwanafalsafa wa karne ya 20. “Maoni ya kisiasa ya Aristotle yalitegemea serikali za jiji za Ugiriki zilizokuwa zikielekea kutoweka.” Ile dhana ya serikali ndogo ya jiji haingemvumtia mwana-mfalme mwenye kutaka makuu aliyetaka kujenga milki kubwa yenye utawala mmoja. Lazima Aleksanda alitilia shaka sera ya Aristotle ya kuwatumikisha wasio Wagiriki kwa kuwa alitarajia milki yenye ushirikiano mzuri kati ya washindi na washinde.

      Hata hivyo, hakuna shaka kwamba Aristotle alikuza kupendezwa kwa Aleksanda katika kusoma na kujifunza. Aleksanda aliendelea kuwa msomaji mwenye bidii katika maisha yake yote, akipendezwa hasa na maandishi ya Homer. Yadaiwa kwamba alikariri mistari yote 15,693 ya shairi liitwalo Iliad.

      Kuelimishwa na Aristotle kulikoma ghafula mwaka wa 340 K.W.K. wakati ambapo mwana-mfalme huyo mwenye umri wa miaka 16 alirudi Pella akatawale Makedonia kwa kuwa baba yake hakuwako.

  • Ni Nani Atakayeutawala Ulimwengu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • Aristotle na mwanafunzi wake Aleksanda

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki