-
Desturi za Kale Katika Mexico ya LeoAmkeni!—2008 | Machi
-
-
Kwa mfano, kila mwaka, Novemba 2, watu wengi huko Mexico huenda kwenye makaburi ili kukumbuka Siku ya Nafsi Zote, ambayo pia inaitwa Siku ya Wafu. Wao huwaachia wapendwa wao waliokufa maua, chakula, na kileo. Wengine hata hupanga wanamuziki wacheze nyimbo ambazo wapendwa wao walipenda kusikiliza. Pia Wakatoliki wengi hujenga madhabahu katika nyumba zao na wanaweza kuweka picha za mpendwa wao aliyekufa.
Kichapo Enciclopedia de México kinasema kwamba inaonekana mazoea fulani yaliyohusu sherehe za wafu “yana mambo fulani yaliyokuwa katika sherehe za Wenyeji wa Asili wa Amerika zilizofanywa katika miezi ya ochpaniztli na teotleco, wakati ambapo maua ya cempasúchil na vyakula vilivyotengenezwa kwa unga wa mahindi vilitolewa kwa manes [roho za wafu] wakati ambapo mavuno yangekuwa yamekusanywa, yaani, mwishoni mwa Oktoba na mwanzoni mwa Novemba.” Kama ensaiklopidia hiyo inavyoonyesha, desturi fulani hufuata sherehe zinazofanana na zile zilizokuwapo wakati wa kipindi cha kabla ya Wahispania, ambazo zilitia ndani sherehe zenye shamrashamra.
-
-
Desturi za Kale Katika Mexico ya LeoAmkeni!—2008 | Machi
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Wanamuziki makaburini siku ya Novemba 2
-