-
Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?Amkeni!—2007 | Novemba
-
-
Je, Waliweza Kusoma na Kuandika?
Biblia inaonyesha kwamba Waisraeli wa kale walijua kusoma na kuandika. (Hesabu 5:23; Yoshua 24:26; Isaya 10:19) Wachambuzi hawakukubali jambo hilo, wakisema kwamba historia ya Biblia hasa ilipitishwa kwa mdomo kwa njia isiyoweza kutegemeka. Lakini mnamo 2005, wataalamu wa vitu vya kale waliofanya kazi Tel Zayit, eneo lililo kati ya Yerusalemu na Mediterania, walipata herufi za Kiebrania [6] za zamani zaidi kuwahi kugunduliwa, herufi hizo zilikuwa zimeandikwa kwa kuchongwa kwenye mwamba wa chokaa.
Wasomi fulani wanasema kwamba mwamba huo, unaosemekana kuwa wa karne ya kumi K.W.K., unadokeza “mafunzo ya uandishi,” “utamaduni wa hali ya juu,” na “usimamizi wa Kiisraeli uliokuwa ukisitawi huko Yerusalemu.” Tofauti kabisa na madai ya wachambuzi, inaonekana kwamba kufikia angalau mapema katika karne ya kumi K.W.K., Waisraeli waliweza kusoma na kuandika na hivyo wangeweza kurekodi historia yao.
-
-
Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?Amkeni!—2007 | Novemba
-
-
6: AP Photo/Keith Srakocic;
-