Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MAENDELEO NCHINI SAMOA YA MAREKANI

      Kabla ya muda wa akina Sellars kukaa nchini Samoa kumalizika katika mwaka wa 1954, Ron aliamua kutuma maombi yao ya kuwa wakazi nchini Samoa ya Marekani badala ya kurudi Australia. Ron anaandika: “Nilipozungumza na mwanasheria mkuu wa Samoa ya Marekani na kumweleza kwamba serikali ya Samoa ilikuwa imekataa maombi yetu kwa sababu za kidini, aliniambia, ‘Bwana Sellars, tuna uhuru wa kidini nchini Samoa ya Marekani, nitafanya juu chini mpaka mpate vibali hivyo.’”

      Ron na Dolly waliwasili mji wa Pago Pago, nchini Samoa ya Marekani mnamo Januari 5, 1954. Mwanasheria huyo aliwapa vibali vya kuingia kwa sharti moja, kwamba Ron awe akiripoti ofisini kwake mara kwa mara na kumweleza mengi zaidi kuwahusu Mashahidi wa Yehova. Hivyo, wakawa na mazungumzo mengi mazuri ya Biblia.

      Baadaye mwezi huo, mwanasheria huyo aliwaalika Ron na Dolly nyumbani kwake kwa ajili ya chakula. Kwa kuwa padri wa Katoliki na padri wa London Missionary Society walikuwa wamealikwa pia, kukawa na mazungumzo ya Biblia yenye kusisimua. Ron anakumbuka: “Tulipokaribia kuondoka, mwanasheria huyo alitushukuru sote kwa kufika na kusema, ‘Nafikiri Bwana na Bibi Sellars ndio washindi katika mazungumzo yetu leo.’ Muda si muda, tukapata vibali vyetu vya kuwa wakazi wa kudumu. Mwanasheria mkuu aliponijulisha baadaye kwamba serikali ingekubali maombi zaidi ya wamishonari Mashahidi nchini, niliijulisha ofisi ya tawi ya Australia bila kukawia.”

      Ualesi (Wallace) Pedro, Mtokelau mwenye umri wa miaka 19, ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza nchini Samoa ya Marekani kujiweka wakfu kwa Yehova. Lydia Pedro, mtu wao wa ukoo aliyekuwa painia wa pekee huko Fiji, alikuwa amemwachia ndugu ya Wallace kitabu “Let God Be True,” alipowatembelea mwaka wa 1952. Wallace alikipata kitabu hicho nyumbani kwa ndugu yake na kukisoma kwa makini.

      Baada ya kukutana na familia ya Pedro mwaka wa 1954, Ron na Dolly walijifunza na dada na ndugu mkubwa wa Wallace. Wallace alimwamini Yehova Mungu, lakini kwa sababu ya kushuku dini, mwanzoni aliogopa kujiunga na wengine katika funzo. Muda si muda, alisadiki kwamba Mashahidi wa Yehova wanafundisha kweli, naye akaanza kuhudhuria mikutano kwa ukawaida Fagatogo. Alifanya maendeleo ya haraka ya kiroho na mnamo Aprili 30, 1955, Wallace akabatizwa katika Bandari ya Pago Pago.

      Kufikia Januari 1955, mwaka mmoja tu baada ya Ron na Dolly kufika, watu saba walikuwa wakihudhuria mikutano katika nyumba ndogo ya painia katika kijiji cha Fagatogo. Kwa sababu ya uhaba wa viti, watu waliketi sakafuni. Muda si muda, watatu kati yao walianza kuandamana na Ron na Dolly katika huduma ya shambani. Ijapokuwa ilikuwa siku ya mambo madogo, kulikuwa na mengi akibani.

  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 87]

      “Nilifurahi Kila Siku”

      RONALD SELLARS

      ALIZALIWA 1922

      ALIBATIZWA 1940

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Yeye na mke wake, Olive (Dolly), walifika Samoa wakiwa mapainia wa pekee mwaka wa 1953. Alihitimu shule ya wamishonari ya Gileadi mwaka wa 1961. Ron bado anatumikia akiwa painia wa pekee huko Samoa ya Marekani.

      SERIKALI ya Samoa ilipokataa kuongeza muda wetu wa kukaa, mimi na Dolly tulihamia Samoa ya Marekani. Tulishushwa na meli kwenye gati la mji wa Pago Pago saa tisa alfajiri, wakati ambapo hakukuwa na watu. Hakukuwa na wahubiri wengine katika nchi hiyo nasi tulikuwa na dola 12 tu mfukoni. Baadaye asubuhi hiyo, baba ya mtu ambaye awali alikuwa akijifunza Biblia alitupa mahali pa kukaa. Alikuwa na chumba kimoja, nasi tulikuwa tukilala kwenye kona, iliyotengwa kwa pazia. Ingawa tulitaka kutafuta nyumba ya kukaa, tulianza kuhubiri nyumba ya jirani yake.

      Majuma kadhaa baadaye, tulikodisha nyumba kubwa iliyokuwa juu ya duka la jumla katika kijiji cha Fagatogo. Ukiwa katika nyumba hiyo, ungeweza kuona vizuri Bandari ya Pago Pago hata hivyo ilikuwa tupu. Ndugu Knorr alikuwa ametuambia: “Mtakapoenda kwenye visiwa vya Pasifiki, huenda maisha yakawa magumu. Huenda mkalazimika kutandaza makatoni ya vitabu sakafuni na kuyatumia kama kitanda.” Hivyo ndivyo tulivyofanya! Miezi mingi ilipita kabla hatujapata pesa za kutosha kutengeneza kitanda, meza, na viti vinavyofaa. Hata hivyo, tulifurahi kuwa na nyumba yetu wenyewe.

      Ingawa mke wangu mpendwa alikufa mwaka wa 1985, bado mimi huenda katika utumishi wa shambani siku nyingi. Ninapofikiria miaka zaidi ya 50 ambayo nimetumia katika utumishi wa upainia na umishonari, kwa kweli ninaweza kusema kwamba nilifurahi kila siku!

  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Baadaye nikamwoa Caroline Hinsche, painia mwenye bidii kutoka Kanada aliyekuwa akitumikia nchini Fiji, nasi tukawa mapainia wa pekee nchini Samoa ya Marekani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki