-
Samoa2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 109, 110]
“Hatukuchoka Kurudi”
FRED WEGENER
ALIZALIWA 1933
ALIBATIZWA 1952
MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Yeye pamoja na mke wake Shirley, wanatumikia katika Betheli ya Samoa. Fred ni mshiriki wa Halmashauri ya Nchi.
BAADA ya kufunga ndoa mwaka wa 1956, tulihamia Samoa ya Marekani kutoka Australia ili kutumikia tukiwa mapainia wa pekee. Mgawo wetu wa kwanza ulikuwa Lauli‘i, kijiji kidogo kilicho upande wa mashariki wa Bandari ya Pago Pago. Huko, tulianza kuishi katika kibanda kibovu, ambacho hakikikuwa na milango, madirisha, paa, wala maji ya bomba. Baada ya kukikarabati kidogo, familia yetu ikaongezeka. Wallace Pedro, kijana mwenyeji aliyekuwa amefukuzwa nyumbani na wazazi wake, akaanza kuishi na kuhubiri pamoja nasi.
-
-
Samoa2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Miaka minane baadaye, mwana wetu Darryl alizaliwa, nasi tukaacha kuzunguka na kukaa Samoa ya Marekani. Nilitumikia nikiwa painia wa pekee, naye Shirley alitumia muda wake mwingi akitafsiri vitabu na magazeti ya Biblia katika Kisamoa.
Wakati huo pia, nilifanya kazi pamoja na Shahidi mzamia koa ili kukimu mahitaji ya familia. Mtambo wa mashua yake uliharibika, nasi tukakaa baharini kwa siku nne. Mawimbi yalitupeleka mamia ya kilomita, tukakumbwa na dhoruba kali, tukaona meli 32 zikipita, na hata karibu tugongwe na meli kubwa ya makontena kabla ya kuokolewa. Muda mfupi baadaye, Shirley nami tukagundua kwamba tunatarajia kupata mtoto mwingine. Kwa hiyo, mwaka wa 1974, tukaamua shingo upande kurudi Australia, ambako binti yetu, Tamari, alizaliwa.
-