-
Kuvutiwa Sana na MalaikaAmkeni!—1999 | Novemba 22
-
-
Mamia ya Vitabu
Kisha kuna vitabu. Duka moja kubwa la vitabu katika New York City huuza zaidi ya aina 500 za vitabu vinavyozungumzia malaika, hasa malaika-walinzi. Vitabu vya aina hii huahidi kuwaonyesha wasomaji jinsi ya kuwasiliana na malaika-walinzi, kujifunza majina yao, kuongea nao, na kupata msaada wao. Vitabu hivyo huwa na masimulizi mengi ya jinsi ambavyo malaika wameonekana wakati wa uhitaji, wakiwanusuru watu kutokana na magari yaliyoko barabarani, kutibu maradhi hatari, kufariji wanaosononeka, na kuwalinda askari-jeshi katika uwanja wa mapigano. Malaika hao hutumikia “bila kudai ishara ya kutubu, kugeuzwa imani, au ya kuwa mwaminifu kwa mafundisho ya kidini.” Lakini masimulizi haya ya kisasa ya “kukutana na malaika” huchochea watu kwa nadra sana wafanye mabadiliko maishani mwao. Kwa kawaida wale wanaodai walikutana na malaika huwa tu na hisia changamfu.
-
-
Kuthibitisha Masimulizi HayoAmkeni!—1999 | Novemba 22
-
-
Kitabu Angels—An Endangered Species huorodhesha ufanani kati ya masimulizi haya, kikidai kwamba yote yaweza kuwa na fasili moja.b Ufuatao ni muhtasari wa baadhi ya ufanani ulioorodheshwa katika kitabu hicho.
1. Malaika na viumbe wasiotambuliwa hutoka katika ulimwengu mwingine.
2. Wote ni viumbe bora, ama kiroho ama kitekinolojia.
3. Jamii yenye urafiki kati yao huonekana ikiwa na ujana na yenye umbo maridadi, na ni yenye fadhili na huruma nyingi.
4. Hawana tatizo la lugha, wao husema kwa ufasaha lugha ya msikilizaji.
5. Wote ni stadi wa kuruka hewani.
6. Malaika na viumbe wasiotambuliwa huonekana wakiwa na nuru nyangavu.
7. Wote huonekana wakiwa na mavazi kamili, kwa kawaida wanavaa kanzu au makoti marefu yenye kubana. Wanapenda mavazi ya rangi nyeupe au ya buluu.
8. Kwa kawaida wote huwa na kimo sawa na wanadamu.
9. Wote huhangaikia hali mbaya ya wanadamu na sayari yao.
10. Uthibitisho wa kukutana na malaika au na viumbe wasiotambuliwa ni ushuhuda wa mtu aliyewaona.
-