-
Imani Yao Ilishinda Jaribu KaliSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
WATUPWA NDANI YA TANURU YENYE MOTO!
18, 19. Ni nini kilichotukia Waebrania hao watatu walipotupwa kwenye tanuru yenye moto?
18 Nebukadreza mwenye ghadhabu akaamuru kwamba watumishi wake waipashe moto tanuru, mara saba zaidi ya kawaida. Kisha akaamuru “baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake” kuwafunga Shadraka, Meshaki, na Abednego na kuwatupa kwenye “tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.” Walitekeleza maagizo ya mfalme, wakawatupa Waebrania hao watatu motoni, wakiwa wamefungwa na wakiwa na mavazi yao—huenda ili wachomeke haraka zaidi. Hata hivyo, mashujaa wa Nebukadreza wenyewe ndio waliouawa na miali ya moto.—Danieli 3:19-22.
19 Lakini jambo la ajabu lilikuwa likitukia. Ingawa Shadraka, Meshaki, na Abednego walikuwa katikati ya tanuru yenye moto, miali haikuwa ikiwachoma. Nebukadreza alipigwa na butaa kama nini! Walikuwa wametupwa kwenye moto mkali, wakiwa wamefungwa kwa nguvu, lakini bado walikuwa hai. Hata walikuwa wakitembea-tembea tu motoni! Lakini Nebukadreza aliona kitu kingine. “Je! hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto?” akauliza mawaziri wake wa makao ya kifalme. “Kweli, Ee mfalme,” wakajibu. “Tazama,” Nebukadreza akapaaza sauti, “mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.”—Danieli 3:23-25.
20, 21. (a) Nebukadreza aliona nini juu ya Shadraka, Meshaki, na Abednego walipotoka kwenye tanuru? (b) Nebukadreza alilazimika kukiri nini?
20 Nebukadreza akaukaribia mlango wa tanuru yenye moto. “Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu,” akawaita kwa sauti, “tokeni, mje huku.” Waebrania hao watatu wakatoka motoni. Haikosi watu wote waliojionea muujiza huo—kutia ndani maamiri, manaibu, maliwali, na mawaziri—waliduwaa. Kwani, ilikuwa kana kwamba vijana hao watatu hata hawakuwa wameingia kamwe ndani ya tanuru! Hawakuwa na harufu ya moto, na hakuna hata unywele wa vichwa vyao uliokuwa umechomeka.—Danieli 3:26, 27.
21 Sasa Mfalme Nebukadreza alilazimika kukiri kwamba Yehova ndiye Mungu Aliye Juu. “Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego,” akatangaza, “aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.” Kisha mfalme akaongezea onyo hili kali: “Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.” Basi, Waebrania hao watatu wakapendelewa tena na mfalme, ‘wakakuzwa katika wilaya ya Babeli.’—Danieli 3:28-30.
-
-
Imani Yao Ilishinda Jaribu KaliSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 78]
-