Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Anafunua Mambo Ambayo “Lazima Yatendeke Upesi”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 15
    • Kufikia karne ya 17, Uingereza ilikuwa serikali isiyo na nguvu sana. Nchi nyingine tatu katika Milki ya kale ya Roma, yaani, Hispania, Uholanzi, na Ufaransa, zilikuwa na uvutano zaidi. Uingereza iling’oa serikali hizo moja baada ya nyingine, ikaziondoa kwenye vyeo hivyo vya kifahari. Kufikia katikati ya karne ya 18, Uingereza ilikuwa ikielekea kuwa serikali kuu ya ulimwengu. Lakini bado haikuwa kichwa cha saba cha yule mnyama-mwitu.

      5 Ingawa Uingereza ilipata mamlaka, nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wake huko Amerika Kaskazini zilijitenga. Hata hivyo, Uingereza haikuizuia Marekani kuendelea kupata nguvu, na Marekani ililindwa na jeshi la wanamaji la Uingereza. Siku ya Bwana ilipoanza mwaka wa 1914, Uingereza ilikuwa imejenga milki kubwa zaidi katika historia na Marekani ilikuwa sasa nchi iliyositawi zaidi kiviwanda duniani.b Wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, Marekani ilikuwa imesitawisha uhusiano wa pekee na Uingereza. Kichwa cha saba cha yule mnyama sasa kilikuwa kimeibuka kikiwa Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani.

  • Yehova Anafunua Mambo Ambayo “Lazima Yatendeke Upesi”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 15
    • b Ingawa nchi ya Uingereza na Marekani ambazo zinafanyiza serikali hiyo pacha ya ulimwengu zimekuwapo tangu karne ya 18, Yohana anaeleza jinsi ambavyo zingetokea mwanzoni mwa siku ya Bwana. Kwa kweli, maono yaliyoandikwa katika kitabu cha Ufunuo yanatimia katika “siku ya Bwana.” (Ufu. 1:10) Kichwa cha saba kilianza kutenda kama serikali kuu ya ulimwengu ya muungano wakati tu wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki