-
Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
Mshindi wa tuzo la Nobeli aliye mwanasayansi wa ubongo, Sir John Eccles aliandika: “Hakuna eneo lolote linalolingana . . . na eneo la usemi la Broca ambalo limetambuliwa katika nyani.” Hata kama sehemu nyinginezo zinazofanana na hizo zinapatikana katika wanyama, ukweli ni kwamba wanasayansi hawawezi kuwafundisha nyani watokeze usemi ila tu sauti chache tu rahisi. Lakini, wewe unaweza kutokeza lugha yenye mambo mengi sana. Ili kufanya hivyo, unapanga maneno yako kulingana na sarufi ya lugha yako. Eneo la Broca hukusaidia kufanya hivyo, katika usemi na katika maandishi.
-
-
Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
Kuna tofauti kubwa kama nini kati ya jinsi nyani atumiavyo ishara na uwezo mkubwa wa lugha ya watoto! Sir John Eccles alirejezea kile ambacho wengi wetu tumeona, uwezo “udhihirishwao na hata watoto wenye umri wa miaka 3 waulizapo maswali mengi wakitaka kuelewa mambo mengi wanayoyaona.” Yeye aliongezea: “Kwa kutofautisha, nyani hawaulizi maswali.” Ndiyo, ni wanadamu pekee waulizao maswali, kutia ndani maswali kuhusu maana ya maisha.
-
-
Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 59]
Lugha na Akili
Kwa nini akili ya binadamu inashinda sana akili ya wanyama, kama vile nyani? Jambo kubwa ni uwezo wetu wa kuunganisha sauti kufanyiza maneno na kutumia maneno kufanyiza sentensi. Mtaalamu wa utendaji wa ubongo Dakt. William H. Calvin aeleza:
“Sokwe wasiofugwa hutoa karibu dazani tatu za sauti tofauti-tofauti ili kuwasilisha karibu dazani tatu za maana tofauti-tofauti. Wao waweza kurudia sauti ili kukazia maana, lakini wao hawaunganishi sauti tatu tofauti-tofauti ili kufanyiza neno jipya katika msamiati wao.
“Sisi wanadamu pia hutumia karibu dazani tatu za sauti, ambazo huitwa fonimi. Lakini ni miunganisho ya hizo ndiyo hutokeza maana: sisi huunganisha sauti zisizo na maana ili kuunda maneno yenye maana.” Dakt. Calvin alitaja kwamba “hakuna mtu ambaye ameeleza sababu ya kuwako kwa” tofauti kubwa sana kati ya “sauti moja/maana moja” ya wanyama na uwezo mkubwa wa ajabu wa mwanadamu wa kuunda maneno.
-