Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ule Uasi-Imani Mkubwa

      10. Ni jambo gani lililoupata mfumo wa Kiyahudi na wategemezaji wao wasiotubu katika 70 W.K.?

      10 Wakati Yohana alipoandika Ufunuo, Ukristo ulikuwa na umri wa zaidi ya miaka 60. Mwanzoni, ulikuwa umeokoka miaka 40 ya upinzani wa daima kutoka dini ya Kiyahudi. Kisha mfumo wa Kiyahudi ukapokea pigo la kifo katika 70 W.K. wakati Wayahudi wasiotubu walipopoteza utambulishi wao wa kuwa taifa pamoja na kile ambacho kwao kilikaribia sana kuwa sanamu ya kuabudiwa—lile hekalu katika Yerusalemu.

      11. Kwa nini ilifaa sana yule Mchungaji Mkuu ayaonye makundi juu ya miendo iliyokuwa ikisitawi?

      11 Hata hivyo, mtume Paulo alikuwa ametabiri kwamba kungekuwako uasi-imani miongoni mwa Wakristo wapakwa-mafuta, na jumbe za Yesu huonyesha kwamba katika umri wa uzee wa Yohana uasi-imani huu ulikuwa tayari ukisitawi. Yohana alikuwa wa mwisho wa wale waliokuwa wakitenda wakiwa kizuizi katika jaribio hili la kupindukia la Shetani la kufisidi ile mbegu ya mwanamke. (2 Wathesalonike 2:3-12; 2 Petro 2:1-3; 2 Yohana 7-11) Kwa hiyo ulikuwa wakati unaofaa kwa Mchungaji Mkuu wa Yehova kuandikia wazee katika makundi, akiwaonya juu ya miendo iliyokuwa ikisitawi na kuwatia moyo wale wenye mioyo iliyo sawa wasimame imara kwa ajili ya uadilifu.

      12. (a) Ule uasi-imani ulisitawije katika karne za baada ya siku ya Yohana? (b) Jumuiya ya Wakristo ilipataje kuwako?

      12 Sisi hatujui jinsi makundi yalivyoitikia jumbe za Yesu katika 96 W.K. Lakini tunalojua ni kwamba ule uasi-imani ulisitawi kwa haraka sana baada ya kifo cha Yohana. “Wakristo” waliacha kutumia jina Yehova na badala yalo wakaweka “Bwana” au “Mungu” katika hati za Biblia.

  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Yesu alikuwa amelionya kundi katika Pargamamu juu ya kufanyiza mafarakano. Hata hivyo, mafarakano yalitokea hata katika karne ya pili, na leo Jumuiya ya Wakristo ina maelfu ya mafarakano na dini zenye kuzozana.—Ufunuo 2:15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki