Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufumbua Fumbo la Ule Mti Mkubwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • Lakini vipi juu ya utimizo mkubwa wa ndoto yake? Zile “nyakati saba” za kiunabii zilikuwa ndefu kuliko siku 2,520. Hilo lilionyeshwa na maneno ya Yesu: “Yerusalemu litakanyagwa-kanyagwa na mataifa, hadi nyakati zilizowekwa rasmi za mataifa ziwe zimetimizwa.” (Luka 21:24) ‘Kukanyaga-kanyaga’ huko kulianza mwaka wa 607 K.W.K. wakati ambapo Yerusalemu liliharibiwa nao ufananisho wa ufalme wa Mungu ukakoma kutenda katika Yuda. Kukanyaga-kanyaga huko kungekoma lini? Kungekoma “nyakati za kurudishwa kwa mambo yote,” wakati ambapo enzi kuu ya Mungu ingedhihirishwa tena kwenye dunia kupitia Yerusalemu la ufananisho, Ufalme wa Mungu.—Matendo 3:21.

      27. Kwa nini ungesema kwamba zile “nyakati saba” ambazo zilianza mwaka wa 607 K.W.K. hazikuisha siku 2,520 halisi baadaye?

      27 Ikiwa tungehesabu siku halisi 2,520 kuanzia kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K., tungefikia mwaka wa 600 K.W.K., mwaka usio na maana yoyote ya Kimaandiko. Hata mwaka wa 537 K.W.K., wakati ambapo Wayahudi waliowekwa huru walirudi Yuda, enzi kuu ya Yehova haikuwa duniani. Na hiyo ni kweli kwa kuwa Zerubabeli, mrithi wa kiti cha Daudi, hakufanywa mfalme bali liwali tu wa Yuda, mkoa wa Uajemi.

      28. (a) Ni kanuni gani ambayo lazima itumiwe kuhusu zile siku 2,520 za zile “nyakati saba” za kiunabii? (b) “Nyakati saba” za kiunabii zilikuwa na urefu gani, nazo zilianza na kuisha tarehe gani?

      28 Kwa kuwa zile “nyakati saba” ni za kiunabii, lazima tutumie kanuni ya Kimaandiko kwenye zile siku 2,520: “Siku moja kwa mwaka mmoja.” Kanuni hiyo yatumika kwenye hali ya Babiloni kuzingira Yerusalemu. (Ezekieli 4:6, 7; linganisha Hesabu 14:34.) Kwa hiyo, zile “nyakati saba” za serikali za wasio Wayahudi kutawala dunia bila kuingiliwa na Ufalme wa Mungu zilikuwa na urefu wa miaka 2,520. Zilianza wakati ambapo Yuda na Yerusalemu zilifanywa ukiwa katika mwezi wa saba unaofuata kuandama kwa mwezi (Tishri 15) mwaka wa 607 K.W.K. (2 Wafalme 25:8, 9, 25, 26) Kuanzia wakati huo hadi mwaka wa 1 K.W.K. ni miaka 606. Ile miaka iliyosalia 1,914 yaanza kutoka wakati huo hadi mwaka wa 1914 W.K. Kwa hiyo, “nyakati saba,” au miaka 2,520, ziliisha kufikia Tishri 15, au Oktoba 4/5, 1914 W.K.

      29. “Mnyonge” ni nani, na Yehova alifanya nini ili kumtawaza?

      29 Mwaka huo “nyakati zilizowekwa rasmi za mataifa” zilitimia, na Mungu akampa utawala “mnyonge”—Yesu Kristo—ambaye adui zake walimwona kuwa mnyonge sana hivi kwamba wakafanya atundikwe mtini. (Danieli 4:17)

  • Kufumbua Fumbo la Ule Mti Mkubwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • NYAKATI SABA ZINAZOTUATHIRI

      24. (a) Ule mti mkubwa wa ndoto wawakilisha nini? (b) Ni nini kilichozuiwa kwa nyakati saba, na hilo lilitokeaje?

      24 Kama alivyowakilishwa na ule mti mkubwa, Nebukadreza alifananisha utawala wa ulimwengu. Lakini kumbuka kwamba ule mti unawakilisha utawala na enzi kuu iliyo kubwa kuliko utawala wa mfalme wa Babiloni. Mti huo wafananisha enzi kuu ya ulimwengu wote ya Yehova, “Mfalme wa mbinguni,” hasa kuhusiana na dunia. Kabla ya Yerusalemu kuharibiwa na Wababiloni, ufalme uliokuwa katika jiji hilo, Daudi na warithi wake wakikalia “kiti cha enzi cha BWANA,” uliwakilisha enzi kuu ya Mungu kuhusiana na dunia. (1 Mambo ya Nyakati 29:23) Mungu mwenyewe alifanya enzi hiyo kuu ikatwe na kufungwa pingu mwaka wa 607 K.W.K. alipomtumia Nebukadreza kuharibu Yerusalemu. Utawala wa Mungu duniani kupitia ufalme wa nasaba ya Daudi ulizuiliwa kwa nyakati saba. Nyakati hizo saba zilikuwa na urefu gani? Zilianza lini, na ni nini kilichoonyesha mwisho wake?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki