Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Vigae vya Kale Vinaunga Mkono Masimulizi ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Novemba 15
    • Vigae vya Aradi

      Aradi lilikuwa jiji la kale lililokuwa katika eneo kame lililoitwa Negebu, kusini mwa Yerusalemu. Eneo la Aradi lilipochimbuliwa kulipatikana ngome sita za Waisraeli zilizofuatana tangu wakati wa ufalme wa Sulemani (1037-998 K.W.K.) mpaka Yerusalemu lilipoharibiwa na Wababiloni katika 607 K.W.K. Huko Aradi, wachimbuaji walipata vigae vingi zaidi vya tangu nyakati za Biblia. Vigae hivyo vinatia ndani vipande zaidi ya 200 vyenye maandishi ya Kiebrania, ya Kiaramu, na ya lugha nyinginezo.

      Baadhi ya vigae vya Aradi vinaunga mkono masimulizi ya Biblia kuhusu familia za kikuhani. Kwa mfano, kigae kimoja kinawataja “wana wa Kora” wanaotajwa katika Kutoka 6: 24 na Hesabu 26:11. Utangulizi wa Zaburi 42, 44-49, 84, 85, 87, na 88 unasema waziwazi kuwa zaburi hizo zilitungwa na “wana wa Kora.” Familia nyingine za kikuhani zinazotajwa na vigae vya Aradi ni zile za Pashuri na Meremothi.—1 Mambo ya Nyakati 9:12; Ezra 8:33.

      Fikiria mfano mwingine. Katika magofu ya ngome inayosemwa kuwa ya kipindi kilichotangulia tu kuharibiwa kwa Yerusalemu na Wababiloni, wachimbuaji walipata kigae alichoandikiwa kamanda wa ngome. Kichapo fulani (The Context of Scripture) kinasema hivi kwa sehemu: “Kwa bwana wangu Elyashib. Yahweh [Yehova] na ahangaikie hali njema yako. . . . Kuhusu mambo uliyoniagiza: kila jambo liko sawa sasa: anakaa katika nyumba ya Yahweh.” Wasomi wengi wanaamini kwamba hekalu linalozungumziwa ni hekalu la Yerusalemu, ambalo lilijengwa kwanza katika siku za Sulemani.

  • Vigae vya Kale Vinaunga Mkono Masimulizi ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Novemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 13]

      Kigae kutoka katika magofu ya Aradi ambacho mtu anayeitwa Elyashib aliandikiwa

      [Hisani]

      Photograph © Israel Museum, Jerusalem; courtesy of Israel Antiquities Authority

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki