Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwaka Mmoja Katika “Nchi Nzuri”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Juni 15
    • MWAKA wa 1908, kitu fulani chenye kuvutia kiligunduliwa katika eneo la jiji la Gezeri linalotajwa katika Biblia ambalo liko karibu na eneo tambarare la pwani magharibi ya Yerusalemu. Kitu kilichogunduliwa katika eneo hilo ni bamba dogo la jiwe la chokaa ambalo linaaminika kuwa la karne ya kumi K.W.K. Kwenye bamba hilo, kuna maandishi ya kale ya Kiebrania, ambayo yana kile kinachofikiriwa kuwa chati ya mwaka au mzunguko wa kilimo ambayo haina maelezo mengi, lakini inaonyesha shughuli zote za kilimo. Baadaye, bamba hilo liliitwa Kalenda ya Gezeri.

      Bamba hilo lina jina: Abiya. Wataalamu wengi wa vitu vya kale vilivyochimbuliwa wanaliona bamba hilo kuwa kitabu cha mvulana wa shule kilichoandikwa kama shairi. Lakini wataalamu wengine hawakubaliani na jambo hilo.a

  • Mwaka Mmoja Katika “Nchi Nzuri”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Juni 15
    • a Kalenda ya Gezeri haipatani kabisa na miezi ambayo kwa ujumla ilifuatwa katika Biblia. Zaidi ya hilo, shughuli fulani za kilimo zilitukia nyakati tofauti kidogo katika maeneo mbalimbali ya Nchi ya Ahadi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki