-
Har–MagedoniKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Neno la Kigiriki Har Ma·ge·donʹ, kutoka katika Kiebrania, ambalo hutafsiriwa na watafsiri wengi kuwa “Amagedoni” au “Har–Magedoni,” linamaanisha “Mlima wa Megido” au “Mlima wa Kusanyiko la Vikosi.”
-
-
Har–MagedoniKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Kutumiwa kwa jina Har–Magedoni (Amagedoni) hakumaanishi kwamba vita hivyo vitapiganwa kwenye mlima halisi wa Megido
Hakuna Mlima halisi wa Megido; ila kilima chenye urefu wa meta 21 ambapo magofu ya Megido ya kale yanapatikana.
Wafalme na majeshi ya kivita ya “ulimwengu wote” hayangeweza kutoshea katika Uwanda wa Esdraeloni, chini ya Megido. Uwanda huo ni wenye pembe tatu, urefu wa kilometa 32 tu, na upana wa kilometa 29 upande wa mashariki.—The Geography of the Bible (New York, 1957), Denis Baly, uku. 148.
Jina hilo linafaa kwa sababu ya mambo yaliyokuwa yakitukia huko Megido nyakati za kale; uwanda uliokuwa chini ya Megido ulikuwa mahali pa vita vya kukata maneno
Huko Yehova alimfanya Sisera, yule mkuu wa jeshi la Wakanaani, ashindwe mbele ya Mwamuzi Baraka.—Amu. 5:19, 20; 4:12-24.
Thutmose wa Tatu, farao wa Misri, alisema: “Kuteka Megido ni sawa na kuteka miji elfu!”—Ancient Near Eastern Texts Relating to the Old Testament (Princeton, N.J.; 1969), kilichohaririwa na James Pritchard, uku. 237.
Kurejelewa kwa Megido (maana yake, “Kusanyiko la Vikosi”) kwafaa kwa sababu Har–Magedoni ni hali ya ulimwengu ambayo vikosi vya kijeshi na wote wanaowaunga mkono watawala wa mataifa yote watahusika.
-