Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Har-magedoni—Mwanzo Wenye Furaha
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 1
    • Har-magedoni—Mwanzo Wenye Furaha

      NENO “Har–Magedoni” linatokana na neno la Kiebrania Har–Magedon, au “Mlima wa Megido.” Neno hilo linapatikana kwenye andiko la Ufunuo 16:16 linalosema hivi: “Yakawakusanya pamoja mahali panapoitwa katika Kiebrania Har–Magedoni.”

  • Har-magedoni—Mwanzo Wenye Furaha
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 1
    • Je, kutajwa kwa “Mlima wa Megido” kunamaanisha kwamba Har–Magedoni itapiganwa katika mlima fulani huko Mashariki ya Kati? La. Kwanza kabisa, hakuna mlima unaoitwa hivyo—mahali Megido ya kale ilipokuwa, kuna kilima tu chenye urefu wa meta 20 hivi kando ya bonde. Isitoshe, eneo la Megido haliwezi kuwatosha “wafalme [wote] wa dunia na majeshi yao.” (Ufunuo 19:19) Hata hivyo, Megido lilikuwa eneo ambako baadhi ya vita vikali sana na vya kukata maneno katika historia ya Mashariki ya Kati vilipiganwa. Hivyo, jina Har–Magedoni linawakilisha vita vya kukata maneno, vyenye mshindi mmoja tu.—Ona sanduku “Megido Ni Mfano Unaofaa,” katika ukurasa wa 5.

  • Har-magedoni—Mwanzo Wenye Furaha
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 1
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 5]

      MEGIDO NI MFANO UNAOFAA

      Megido ya kale ilikuwa mahali muhimu sana, karibu na sehemu ya magharibi ya Bonde la Yezreeli lenye rutuba, kaskazini mwa Israeli. Barabara zilizotumiwa na wafanyabiashara na wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali zilifika huko. Hivyo, Megido ikawa mahali pa vita vya kukata maneno. Profesa Graham Davies aliandika hivi katika kitabu chake (Cities of the Biblical World—Megiddo): ‘Wafanyabiashara na wahamiaji kutoka sehemu mbalimbali wangeweza kufika katika jiji la Megido kwa urahisi; lakini wakati ambapo jiji hilo lilikuwa na uwezo, lingeweza kudhibiti njia za kuingia humo na hivyo kusimamia maendeleo ya kibiashara na ya kivita. Kwa hiyo, haishangazi kwamba mara nyingi jiji hilo lilipiganiwa, na walioshinda, walililinda sana.’

      Historia ya jiji la Megido ilianza zaidi ya miaka 3,500 iliyopita, wakati mtawala wa Misri, Thutmose wa Tatu, alipowashinda watawala wa Kanaani huko. Iliendelea kwa karne nyingi hadi mwaka wa 1918 wakati ambapo Jenerali Mwingereza, Edmund Allenby, alipoyashinda majeshi ya Uturuki. Mungu alimwezesha Mwamuzi Baraka kumshinda Mfalme Yabini wa Kanaani huko Megido. (Waamuzi 4:12-24; 5:19, 20) Mwamuzi Gideoni aliwashinda Wamidiani katika eneo hilohilo. (Waamuzi 7:1-22) Pia, Wafalme Ahazia na Yosia waliuawa huko.—2 Wafalme 9:27; 23:29, 30.

      Hivyo, kuhusianisha Har–Magedoni na sehemu hiyo ni jambo linalofaa kwa kuwa Megido ni eneo lililotumiwa kwa ajili ya mapambano mengi ya kukata maneno. Ni mfano unaofaa kuonyesha ushindi kamili wa Mungu juu ya wote wanaompinga.

      [Hisani]

      Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki