Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 2
    Amkeni!—2010 | Desemba
    • Mche wa udongo ulikuwa na maandishi yenye majivuno ya Senakeribu

      Mche wa udongo ulikuwa na maandishi yenye majivuno ya Senakeribu alipovamia Yuda

      Huko Ninawi, wachimbuzi wa vitu vya kale wamepata maandishi ya kihistoria ya Senakeribu yanayosimulia matukio hayohayo. Katika maandishi hayo yaliyoandikwa kwenye mche wa udongo wenye pembe sita, mfalme huyo alijigamba hivi: “Kwa habari ya Hezekia Myahudi, yeye hakujiweka chini ya nira yangu, nilizingira miji 46 kati ya miji yake iliyokuwa imara, ambayo ilikuwa na kuta na ngome, na vijiji vidogo visivyo na hesabu vilivyokuwa karibu, na kushinda (miji na vijiji hivyo) . . . Nilimfanya [Hezekia] awe mfungwa kama ndege kizimbani huko Yerusalemu, makao yake ya kifalme.” Kisha Senakeribu alidai kwamba Hezekia alimpa “talanta 30 za dhahabu, talanta 800 za fedha, mawe yenye thamani, . . . (na) hazina zote zenye thamani,” akitia chumvi idadi ya talanta za fedha alizopokea.

      Hata hivyo, ona kwamba Senakeribu hakusema kwamba alilishinda jiji la Yerusalemu. Hataji hata kidogo jinsi Mungu alivyoangamiza jeshi lake. Biblia inasema kwamba malaika wa Mungu aliwaua wanajeshi 185,000 wa Ashuru katika usiku mmoja. (2 Wafalme 19:35, 36) Msomi Jack Finegan anasema: “Tukizingatia majivuno yanayotajwa kwenye maandishi yote ya wafalme Waashuru, ni wazi kwamba Senakeribu hangeandika kamwe kuhusu ushinde kama huo.”

  • Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 2
    Amkeni!—2010 | Desemba
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki