Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?
    Amkeni!—2007 | Novemba
    • Maandishi ya kihistoria ya Senakeribu [8], yaliyopatikana huko Ninawi, yanafafanua kampeni yake ya kijeshi wakati wa utawala wa Mfalme Hezekia wa Yuda, ambaye maandishi hayo yanamtaja kwa jina. Rekodi zinazopatikana katika mabamba ya wafalme wengine zinawataja Wafalme Ahazi na Manase wa Yuda, na pia Wafalme Omri, Yehu, Yehoashi, Menahemu, na Hoshea wa Israeli.

      Katika masimulizi yake, Senakeribu anajisifu kuhusu mafanikio yake ya kijeshi lakini jambo la kutokeza ni kwamba hataji kwamba alishinda Yerusalemu. Kukosa kutaja jambo hilo kunathibitisha ukweli wa rekodi ya Biblia, ambayo husema kwamba mfalme huyo hakuwahi kuzingira Yerusalemu lakini alishindwa na Mungu mwenyewe. Baada ya hapo, Senakeribu aliyeaibishwa alirudi Ninawi, ambako aliuawa na wanawe. (Isaya 37:33-38) Kwa kupendeza, rekodi mbili za maandishi ya Waashuru zinatoa ushuhuda wa kuuawa kwake.

  • Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?
    Amkeni!—2007 | Novemba
    • 8: Photograph taken by courtesy of the British Museum

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki