-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 2Amkeni!—2010 | Desemba
-
-
Maneno yanayofuata yanaonyesha jinsi mfalme Ashurnasirpal wa Pili wa Ashuru alivyojigamba kuwatendea wote waliompinga:
Mchongo wa mawe unaoonyesha wafungwa wakichunwa ngozi wakiwa hai
“Nilijenga nguzo kwenye lango la jiji lake, na kuwachuna ngozi wakuu wote waliokuwa wameasi, na nikafunika mnara huo kwa ngozi; wengine niliwatundika juu ya mnara, wengine nikawatundika juu ya miti kwenye mnara, . . . na nilikata miguu na mikono ya maofisa, wale maofisa wa kifalme waliokuwa wameasi. . . . Nikachoma kwa moto mateka wengi miongoni mwao, nami nikachukua mateka wengi walio hai.” Wachimbuzi wa vitu vya kale walipochimbua majumba ya kifalme ya Ashuru, walipata kuta zilizorembeshwa kwa michoro ya mateka wakitendewa kinyama.
-