Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
    • 13 Kuhani wa cheo cha juu yumo uani mwa tabenakulo. Baada ya kujiosha kwenye birika la maji, yeye achinja fahali kwa ajili ya dhabihu. Damu ya huyo fahali inamwagwa bakulini; itatumiwa kwa njia ya pekee ili kufunika dhambi za kabila la kikuhani la Lawi. (Mambo ya Walawi 16:4, 6, 11) Lakini kabla ya kuendelea kutoa dhabihu, kuna jambo ambalo kuhani wa cheo cha juu lazima afanye. Yeye achukua uvumba wenye marashi (yaelekea akiuweka ndani ya kijiko cha kupakulia) na makaa-mawe yenye moto kutoka madhabahu ndani ya kishikio cha moto. Sasa aingia ndani ya Patakatifu na kutembea kuelekea lile pazia la Patakatifu Zaidi Sana. Anapita polepole kuzunguka pazia na kusimama mbele ya sanduku la agano. Baadaye, bila kuonekana na mwanadamu mwingine yeyote, anamwaga uvumba kwenye yale makaa-mawe yenye moto, na Patakatifu Zaidi Sana panajawa na wingu lenye kunukia.—Mambo ya Walawi 16:12, 13.

  • “Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
    • Kuhani wa cheo cha juu aondoka Patakatifu pa Patakatifu, atwaa damu ya fahali, na kuingia tena ndani ya Patakatifu Zaidi Sana. Kama ilivyoamuriwa katika Sheria, achovya kidole chake ndani ya hiyo damu na kuinyunyiza mara saba mbele ya kifuniko cha Sanduku. (Mambo ya Walawi 16:14) Halafu arudi uani na kuchinja mbuzi, ambaye ni toleo la dhambi “kwa ajili ya watu.” Aleta kiasi fulani cha damu ya huyo mbuzi ndani ya Patakatifu Zaidi Sana na kufanya jambo lilelile alilofanya na damu ya fahali. (Mambo ya Walawi 16:15) Pia utumishi mwingine mbalimbali muhimu ulifanywa Siku ya Kufunika. Kwa kielelezo, kuhani wa cheo cha juu alipaswa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa pili na kuungama juu yake “uovu wote wa wana wa Israeli.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki