Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kulikabili Hilo Tatizo
    Amkeni!—1997 | Februari 22
    • KWA miaka ambayo imepita matibabu kadhaa yametokezwa kwa ajili ya ADHD. Baadhi yayo yamekazia ulaji. Hata hivyo, uchunguzi fulani unadokeza kwamba viongezwaji vya chakula kwa kawaida havisababishi utendaji wa kupita kiasi na kwamba masuluhisho ya lishe mara nyingi hayana matokeo. Njia nyinginezo za kutibu ADHD ni dawa, kurekebisha mwenendo, na uzoezaji wa kufahamu tatizo hilo.a

      Dawa. Kwa kuwa ADHD kwa wazi huhusisha kasoro ya ubongo, dawa za kurudisha usawaziko ufaao wa kemikali zimethibitika kuwa za msaada kwa wengi.b Hata hivyo, dawa hazichukui mahali pa kujifunza. Hizo zasaidia tu mtoto akaze fikira, zikimpa msingi ambao juu yao aweza kujifunza stadi mpya.

      Watu wazima wengi wenye ADHD wamesaidiwa na dawa pia. Hata hivyo, tahadhari yafaa—kwa vijana na watu wazima—kwa kuwa dawa chochezi zitumiwazo kutibu ADHD zaweza kuraibisha.

      Kurekebisha mwenendo. ADHD ya mtoto haiondolei wazazi wajibu wa kutoa nidhamu. Ingawa huenda mtoto akawa na mahitaji ya kipekee kwa habari hii, Biblia huonya wazazi hivi: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” (Mithali 22:6) Katika kitabu chake Your Hyperactive Child, Barbara Ingersoll ataja: “Mzazi ambaye hujiacha ashindwe na kumwacha mtoto wake mwenye utendaji wa kupita kiasi atende bila kuzuiwa hamsaidii mtoto wake. Kama tu vile mtoto yeyote, mtoto mwenye utendaji wa kupita kiasi ahitaji nidhamu yenye kuendelea yenye staha kwa mtoto akiwa mtu. Hilo lamaanisha mipaka iliyowekwa wazi na thawabu na adhabu zifaazo.”

      Kwa hiyo ni jambo la muhimu kwamba wazazi waandae kanuni thabiti. Zaidi ya hayo, kwapasa kuwa na kawaida yenye kufuatwa sana ya utendaji wa kila siku. Huenda wazazi wakataka kumpa mtoto uhuru wa kutengeneza ratiba hii, kutia ndani wakati wa mgawo wa masomo ya nyumbani, kujifunza, kuoga, na kadhalika. Kisha dumu katika kufuatia ratiba hiyo. Hakikisha kwamba kawaida ya kila siku inafuatwa. Phi Delta Kappan lataja hivi: “Madaktari, wanasaikolojia, maofisa wa shule, na walimu wana wajibu kwa mtoto na kwa wazazi wa mtoto kueleza kwamba kuainishwa ADD au ADHD hakumaanishi kwamba mtoto aweza kufanya chochote bila kutiwa nidhamu, bali badala ya hivyo kuainishwa huko ni elezo liwezalo kuongoza kwenye msaada ufaao kwa mtoto aliye na kasoro hiyo.”

      Uzoezaji wa kufahamu tatizo hilo. Hii yatia ndani kumsaidia mtoto kubadili maoni yake kujihusu na kuhusu tatizo lake. “Watu walio na kasoro ya upungufu wa makini huhisi kwamba ni ‘wasiovutia, wapumbavu, na wasiofaa kitu’ hata ingawa ni wenye kuvutia, wenye akili, na wenye moyo mzuri,” aonelea Dakt. Ronald Goldberg. Kwa hivyo, mtoto aliye na ADD au ADHD ahitaji kuwa na maoni yafaayo ya thamani yake, na ahitaji kujua kwamba matatizo yake ya kukosa makini yaweza kushughulikiwa. Hili ni muhimu hasa wakati wa ubalehe. Kufikia wakati mtoto mwenye ADHD yuko katika umri wa utineja, huenda tayari akawa amepatwa na kejeli nyingi kutoka kwa marika wake, walimu, ndugu zake, na labda hata kutoka kwa wazazi wake. Sasa yeye ahitaji kuweka miradi ya kihalisi na kujichanganua istahilivyo badala ya kujiona kuwa mbaya.

      Njia za matibabu zilizo juu zaweza pia kufuatiwa na watu wazima walio na ADHD. “Marekebisho ni ya muhimu yakitegemea umri,” aandika Dakt. Goldberg, “lakini misingi ya matibabu—dawa mahali pafaapo, kurekebisha mwenendo, na [mazoezi ya] kufahamu tatizo hilo—hubaki ikiwa njia zifaazo kwa muda wote wa maisha.”

  • Kulikabili Hilo Tatizo
    Amkeni!—1997 | Februari 22
    • Hata ikiwa udodosaji unafanywa, wazazi wafanya vyema kupima mazuri na mabaya ya dawa zitakazotumiwa. Ritalin yaweza kuondosha dalili zisizotakwa, lakini yaweza pia kuwa na athari za kando zisizofurahisha, kama vile kukosa kupata usingizi, hangaiko lililoongezeka, na wasiwasi. Hivyo, Dakt. Richard Bromfield atahadharisha dhidi ya kumpa mtoto dawa haraka sana ili tu kumwondoshea dalili zake. “Watoto wengi sana, na watu wazima wengi zaidi, wanapewa Ritalin isivyofaa,” yeye asema. “Kutokana na uzoefu wangu, utumizi wa Ritalin hutegemea hasa uwezo wa wazazi na walimu wa kuvumilia mwenendo wa watoto. Najua kuhusu watoto ambao wamepewa ili kuwatuliza badala ya kushughulikia mahitaji yao.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki