-
Kwa Nini Siwezi Kujifunza?Amkeni!—1996 | Juni 22
-
-
Tania, ambaye sasa yuko katika umri wa miaka ya 20, anatatizika kwa kile kiitwacho Tatizo la Upungufu wa Makini Kutokana na Utendaji wa Kupita Kiasi (ADHD).b Yeye asema: “Nina tatizo kubwa na mikutano ya Kikristo, funzo la kibinafsi, na sala kwa sababu ya ukosefu wangu wa uwezo wa kukaza uangalifu au hata kuketi tuli. Huduma yangu inaathiriwa kwa sababu mimi huruka kutoka kichwa hiki hadi kingine haraka sana hivi kwamba hakuna mtu awezaye kufuatana nami.”
Wakati ambapo halifuatiwi na utendaji wa kupita kiasi, tatizo hilo huitwa Kasoro ya Upungufu wa Makini (ADD). Watu wenye tatizo hili mara nyingi hufafanuliwa kuwa waota-ndoto za mchana. Kuhusu wale wenye ADD, mtaalamu wa mfumo wa neva Dakt. Bruce Roseman alisema: “Wao huketi mbele ya kitabu kwa dakika 45, na hawajifunzi chochote.” Kwa sababu fulani-fulani ni vigumu kwao kukaza fikira.
-
-
Kwa Nini Siwezi Kujifunza?Amkeni!—1996 | Juni 22
-
-
Kwa kawaida wale wenye matatizo ya kujifunza hupewa dawa. Yadaiwa kwamba asilimia 70 hivi ya vijana wenye ADHD ambao wamepewa dawa-chochezi wameitikia. Iwe utakubali tiba ya dawa ni jambo la wewe na wazazi wako kuamua baada ya kufikiria uzito wa tatizo, athari mbaya ziwezazo kutokea, na mambo mengineyo.
-