-
Wazo Hilo Laingia Dini ya Kiyahudi, Jumuiya ya Wakristo, na UislamuNi Nini Hutupata Tunapokufa?
-
-
12-14. Origen na Augustino walitimiza fungu gani katika kuchanganya falsafa ya Plato na Ukristo?
12 Wanafalsafa wawili wa mapema kama hao walifanyiza uvutano mkubwa sana juu ya mafundisho ya Jumuiya ya Wakristo. Mmoja alikuwa ni Origen wa Aleksandria (185-254 W.K.), na mwingine ni Augustino wa Hippo (354-430 W.K.). Kuwahusu, New Catholic Encyclopedia inasema: “Pamoja na Origen tu katika Mashariki na Mt. Augustino katika Magharibi nafsi ilithibitishwa kuwa kitu cha kiroho na wazo la kifalsafa lililofanyizwa kutoka asili yake.” Origen na Augustino waliunda mawazo yao kuhusu nafsi juu ya msingi gani?
-
-
Wazo Hilo Laingia Dini ya Kiyahudi, Jumuiya ya Wakristo, na UislamuNi Nini Hutupata Tunapokufa?
-
-
14 Augustino huonwa na wengi katika Jumuiya ya Wakristo kuwa mfikiri mkubwa wa zamani. Kabla ya kuongoka kuwa “Mkristo” akiwa na umri wa miaka 33, Augustino alikuwa na upendezi mkubwa katika falsafa na alikuja kuwa mfuasi wa mawazo mapya ya Plato.a Hata baada ya kuongoka kwake, alibaki na mawazo mapya ya Plato katika fikira zake. “Akili yake ilikuwa mahali ambapo dini ya Agano Jipya ilikuwa kabisa kabisa yenye kuchanganyika na pokeo la Plato la falsafa ya Kigiriki,” yasema The New Encyclopædia Britannica. New Catholic Encyclopedia yakubali kwamba ‘fundisho la Augustino [kuhusu nafsi], ambalo limekuwa kawaida katika Mashariki kufikia karne ya 12 baadaye, lilitokana na mawazo mapya ya Plato.’
-