-
Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
10. Ni kwa ushindi gani yule Mfalme mwenye kushinda amebariki watu wake “katika kutetea na kuthibitisha kisheria habari njema”?
10 Mfalme wetu mwenye kushinda amebariki pia watu wake wenye bidii kwa kuwaongoza kwenye ushindi mwingi “katika kutetea na kuthibitisha kisheria habari njema” katika mahakama ya sheria na mbele ya watawala. (Wafilipi 1:7; Mathayo 10:18; 24:9, NW) Hiyo imekuwa katika mataifa yote—katika Australia, Ajentina, Kanada, Ugiriki, India, Swazilandi, Swizalandi, Uturuki na mabara mengineyo.
-
-
Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Katika Juni 14, 1943, Mahakama Kuu Zaidi Sana iliamua katika kesi ya Taylor v. Mississippi kwamba Mashahidi hawakutia moyo utovu wa ushikamanifu kwa serikali kwa kuhubiri kwao. Siku iyo hiyo, katika kesi ya West Virginia State Board of Education v. Barnette, Mahakama hiyo ilishikilia kwamba baraza la shule halikuwa na haki ya kufukuza kutoka shuleni watoto wa Mashahidi wa Yehova waliokataa kusalimu bendera. Kesho yake yenyewe, Mahakama Kuu ya Australia iliyojaa iliondoa marufuku ambayo nchi hiyo iliwekea Mashahidi wa Yehova, hiyo ikitangazwa kuwa “isiyo ya haki, bila sababu nzuri na yenye uonevu.”
-