Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Mgeni wetu, R. Bennett Brickell,a alizungumza nasi kuhusu Biblia. Baadaye, nyumba yetu ikawa makao ya Ben wakati wowote alipozuru eneo letu. Sisi sote, kutia ndani Martin na watoto wetu wanne, tulimstahi sana. Martin hakupendezwa na ujumbe wa Biblia, ingawa sikuzote alikuwa mwenye fadhili na mkarimu kwa Mashahidi na hasa kwa Ben.

      Ben alinipa misaada mingi ya kujifunzia Biblia, lakini kulikuwako tatizo moja—sikujua kusoma. Hivyo, kwa saburi Ben aliwasomea watoto pamoja nami Biblia na vichapo vinavyotegemea Biblia, na kuelezea alichokuwa akisoma. Alikuwa tofauti na makasisi kama nini, ambao baada ya kumaliza ibada zao za kidini, hawakutumia hata dakika tano kutufundisha kusoma! Ben alituonyesha kutoka kwa Biblia kwamba Shetani na roho waovu wake ndio waanzilishi wa ushirikina mwingi ambao umenasa jamii ya kibinadamu, kutia ndani watu wangu. Jinsi nilivyokuja kuyathamini maneno haya ya Yesu: “Kweli itawaweka nyinyi huru!”—Yohana 8:32.

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Kwa hiyo Ben alipokuja tena Emerald, niliwatayarisha watoto haraka haraka, na sote tukaandamana naye kwenda kuhubiri. Alinionyesha utoaji sahili na kunifundisha kumtegemea Yehova kupitia sala. Nakiri kwamba utoaji wangu haukuwa mzuri sana, lakini ulitoka moyoni mwangu.

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Ben alijua juu ya mipango yangu ya kwenda Sydney, kwa hiyo alipozuru tena, aliniuliza kama nilikuwa na pesa za kutosha. “Ndiyo!” nikajibu. “Nilipata nauli ya gari-moshi kwa kucheza kamari.” Uso wake uligeuka ukawa mwekundu, na moja kwa moja nikafahamu kwamba nilisema jambo lisilofaa. Nikijitetea kwa haraka, niliongezea: “Una shida gani? Sikuiba kamwe!”

      Alipopata utulivu tena, Ben alieleza kwa njia ya fadhili kwa nini Wakristo hawachezi kamari na kuongezea, kwa uhakikishio: “Lakini si kosa lako. Sikuwa nimekwambia.”

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Ben angezuru kila miezi sita hivi, kwa kuwa Mount Isa ilikuwa sehemu ya eneo lake kubwa la kutoa ushahidi. Ikiwa ingetukia awe mjini wakati wa Ukumbusho wa kifo cha Yesu Kristo—lilikuwa tukio la pekee sana kwa Ben, kwa kuwa alikuwa na tumaini la uhai wa kimbingu—angeuadhimisha pamoja na familia yangu, nyakati fulani chini ya mti.

      Kwa kawaida Ben hakuwa akikaa sana, kwa hiyo mimi na watoto tulihubiri kwa sehemu kubwa tukiwa peke yetu.

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Kutaniko Laanzishwa

      Katika Desemba 1953 kutaniko lilianzishwa katika Mount Isa. Ben aliwekwa rasmi kuwa mwangalizi, na binti yangu Ann na mimi ndio peke yetu tulioshiriki katika huduma. Lakini baada ya muda mfupi Mashahidi wengine walihamia mji huo.

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • a Simulizi lenye kutokeza la maisha ya Ben Brickell lilichapishwa katika Mnara wa Mlinzi la Septemba 1, 1972, ukurasa wa 533-536, (la Kiingereza).

  • Upendo Wangu kwa Dunia Utatoshelezwa Milele
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Kipindi cha mazoezi pamoja na Ben katikati ya miaka ya 1950

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki