Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Imani Yajaribiwa Ulaya Wakati wa Wanazi
    Amkeni!—2003 | Februari 8
    • Mwishoni mwa miaka ya 1920, tulikutana na kijana Myugoslavia, Vinzenz Platajs, ambaye tulimwita Vinko. Yeye aliwasiliana na Wanafunzi wa Biblia. Wakati huo Mashahidi wa Yehova walijulikana kwa jina hilo. Muda mfupi baadaye, Mwanafunzi mmoja wa Biblia alianza kutembelea familia yetu. Kwa kuwa Baba alimzuia Mama kwenda kanisani, Mama alimuuliza Vinko kama ilifaa kumwabudu Mungu nyumbani. Vinko alimwonyesha andiko la Matendo 17:24, linalosema kwamba Mungu “hakai katika mahekalu yaliyofanywa kwa mikono,” na akamwelezea kwamba nyumbani ni mahali panapofaa kumwabudu Mungu. Alipendezwa na akaanza kuhudhuria mikutano katika nyumba za Wanafunzi wa Biblia.

  • Imani Yajaribiwa Ulaya Wakati wa Wanazi
    Amkeni!—2003 | Februari 8
    • Katika mwaka wa 1928, Vinko na dada yangu, Josephine—au Pepi, kama tulivyomwita—walionyesha wakfu wao kwa Yehova kwa kubatizwa katika maji. Baadaye walioana. Mwaka uliofuata binti yao, Fini, alizaliwa huko Liévin. Miaka mitatu baadaye walikubaliwa kuingia katika utumishi wa wakati wote nchini Yugoslavia, ambako kazi ya Mashahidi ilikuwa imewekewa vikazo. Ingawa walipata magumu mengi, shangwe na bidii yao katika utumishi wa Yehova iliendelea bila kufifia. Mfano wao ulinichochea nitamani kuwa mtumishi wa wakati wote.

  • Imani Yajaribiwa Ulaya Wakati wa Wanazi
    Amkeni!—2003 | Februari 8
    • Vinko Ni Mwaminifu Hadi Kifo

      Jeshi la Ujerumani lilifika Yugoslavia katika mwaka wa 1941, na kuwalazimu Pepi na mumewe, Vinko, na binti yao mwenye umri wa miaka 12, Fini, kurudi nyumbani Austria. Wakati huo Mashahidi wengi nchini Austria walikuwa gerezani au kwenye kambi za mateso. Kwa kuwa hawakuwa raia wa taifa lolote—hawakuwa raia wa Ujerumani—walipewa kazi ngumu katika shamba moja huko kusini mwa Austria, karibu na nyumbani kwetu.

      Baadaye, mnamo Agosti 26, 1943, Vinko alikamatwa na polisi wa Gestapo (polisi wa siri wa Nazi). Fini alipojaribu kumuaga baba yake, mkuu wa polisi alimpiga kwa nguvu nyingi na kumwangusha upande wa pili wa chumba. Vinko alihojiwa mara kwa mara na kupigwa vibaya na polisi wa Gestapo, kisha akapelekwa katika Gereza la Stadelheim huko Munich.

      Mnamo Oktoba 6, 1943, nilikamatwa na polisi nikiwa kazini, na kupelekwa katika Gereza la Stadelheim, ambako Vinko alikuwa. Kwa kuwa nilijua Kifaransa vizuri, nilitumiwa kuwatafsiria wafungwa wa kivita wa Ufaransa. Nilipata nafasi ya kuzungumza na Vinko nilipokuwa nikitembea humo gerezani.

      Hatimaye Vinko alihukumiwa kifo. Alishtakiwa kwa kuwapelekea Mashahidi vichapo vya Biblia na kuwapatia msaada wa kifedha wanawake Mashahidi ambao waume zao walikuwa katika kambi za mateso. Alihamishwa hadi gereza lilelile ambamo Willi aliuawa karibu na Berlin na kukatwa kichwa katika Oktoba 9, 1944.

      Pindi ya mwisho ambayo Vinko alikutana na familia yake ilikuwa yenye kuvunja moyo. Alikuwa amefungwa kwa minyororo na kupigwa vibaya, na ilikuwa vigumu kwake kuwakumbatia kwa sababu ya minyororo. Fini alikuwa mwenye umri wa miaka 14 alipomwona baba yake kwa mara ya mwisho. Bado anakumbuka maneno yake ya mwisho: “Fini, mtunze mama yako!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki