-
Makosa Yaliyoanzisha Vita vya UlimwenguAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
Risasi Mbili Zilizobadili Ulimwengu
Kufikia mwaka wa 1914, uhasama kati ya serikali zenye nguvu za Ulaya ulisababisha wasiwasi kati ya mataifa na hivyo kutokeza miungano miwili iliyopingana: Shirikisho la Nchi Tatu, yaani, Austria-Hungaria, Italia, na Ujerumani na Maelewano ya Nchi Tatu, ya Uingereza, Ufaransa, na Urusi. Isitoshe, nchi hizo zilikuwa na mahusiano ya kisiasa na kiuchumi pamoja na nchi nyingine kutia ndani nchi kadhaa za eneo la Balkani.
Wakati huo, eneo linaloitwa Balkani lilikuwa na misukosuko ya kisiasa chini ya utawala wa mataifa hayo makubwa, na lilikuwa limejaa mashirika mengi ya siri yaliyokuwa yakipanga njama za kupata uhuru. Kikundi kidogo cha vijana katika eneo hilo kilipanga njama ya kumwua Dyuki Mkuu wa Austria, Francis Ferdinand, wakati wa ziara yake huko Sarajevo, mji mkuu wa Bosnia, Juni 28.a Kulikuwa na polisi wachache tu wakati huo na hivyo kurahisisha kazi yao. Hata hivyo, wauaji hao hawakuwa na uzoefu mwingi. Kijana mmoja alitupa bomu dogo lakini akakosa kulenga shabaha, na wenzake vilevile walishindwa kutimiza lengo lao wakati ulipofika. Gavrilo Princip, ndiye aliyefaulu, lakini alimwua bila kutarajia. Jinsi gani?
Princip alipomwona dyuki mkuu akimpita bila kuathiriwa na bomu hilo, alijaribu kukaribia gari lake lakini hakufaulu. Akiwa amekata tamaa alivuka barabara na kwenda kwenye mkahawa. Wakati huohuo, dyuki mkuu, akiwa amekasirishwa na jaribio hilo la kumwua, akaamua kutumia njia tofauti. Hata hivyo, dereva wake, ambaye hakujua kwamba mipango imebadilika, akaelekea upande usiofaa na ikambidi ageuze gari. Wakati huohuo, Princip alitoka kwenye mkahawa na kumwona dyuki mkuu akiwa ameketi kwenye gari lake ambalo halijafunikwa likiwa mita 3 tu mbele yake. Princip alikaribia gari hilo na kufyatua risasi mbili, na hivyo kumwua dyuki mkuu na mke wake.b Akiwa mzalendo wa Serbia, huenda Princip hakujua jinsi tendo lake lingeanzisha wimbi la matukio mabaya. Hata hivyo, kuna wengine wanaopaswa kulaumiwa kwa mambo yenye kuogopesha ambayo yangefuata.
-
-
Makosa Yaliyoanzisha Vita vya UlimwenguAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
Wimbi Laanza
Ingawa uchunguzi rasmi haukupata uthibitisho uliohusisha serikali ya Serbia katika mauaji ya dyuki mkuu, Austria ilikuwa imeazimia kukomesha uasi wa Waslavi katika milki hiyo kabisa. Austria ilitaka sana “kufunza Serbia somo,” anasema mwanahistoria J. M. Roberts.
Ili kujaribu kutuliza hali, Nicholas Hartwig, aliyekuwa balozi wa Urusi katika mji mkuu wa Serbia, alijitahidi kufanya pande hizo mbili zikubaliane. Lakini alipatwa na mshtuko wa moyo na akafa alipokuwa akikutana na wajumbe wa Austria. Mwishowe, Julai (Mwezi wa 7) 23, Austria ilitumia Serbia orodha ya matakwa waliyopaswa kutimiza. Kwa sababu Serbia haingekubali matakwa yote, Austria ilikatiza mara moja mahusiano yote nao. Wakati huo muhimu sana, mahusiano ya kidiplomasia yalikoma.
Hata hivyo, bado watu fulani walijaribu kuzuia vita. Kwa mfano, Uingereza ilipendekeza kuwe na kongamano la kimataifa, na kiongozi wa Ujerumani alimsihi maliki wa Urusi asikusanye jeshi. Lakini mambo yakaenda mrama. “Viongozi, majenerali, na mataifa mazima-mazima yalilemewa kabisa na matukio yaliyokuwa yakikaribia,” kinasema kitabu The Enterprise of War.
Julai 28, maliki wa Austria, akiwa amehakikishiwa kwamba Ujerumani itamuunga mkono, alitangaza vita dhidi ya Serbia. Urusi iliunga Serbia mkono na hivyo ikajaribu kutisha Austria kwa kukusanya wanajeshi milioni moja hivi kwenye mpaka wa Austria. Kwa sababu kufanya hivyo kungeacha mpaka wa Urusi na Ujerumani bila ulinzi, maliki wa Urusi aliamuru jeshi lote likusanywe.
Maliki huyo alijaribu kumhakikishia kiongozi wa Ujerumani kwamba hakutaka vita na Ujerumani. Hata hivyo, kukusanywa kwa jeshi la Urusi kulifanya Ujerumani itende kwa kasi, na Julai 31, Ujerumani ilianza kutekeleza mpango wa vita wa Schlieffen, na hivyo ikatangaza vita dhidi ya Urusi Agosti (Mwezi wa 8) 1, na siku mbili baadaye ikatangaza vita dhidi ya Ufaransa. Kwa sababu mipango ya vita ya Ujerumani ilihusisha kupitia Ubelgiji, Uingereza ilionya Ujerumani kwamba itatangaza vita dhidi yake ikiwa ingewaingiza Wabelgiji vitani. Majeshi ya Ujerumani yaliingia Ubelgiji Agosti 4. Sasa vita havingeweza kuepukwa.
-
-
Makosa Yaliyoanzisha Vita vya UlimwenguAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
b Princip alimwua kimakosa mke wa dyuki mkuu. Alikuwa amekusudia kumwua gavana wa Bosnia, Jenerali Potiorek, aliyekuwa ndani ya gari hilo pamoja na dyuki mkuu na mke wake, lakini kitu fulani kilifanya asilenge shabaha.
-
-
Makosa Yaliyoanzisha Vita vya UlimwenguAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
[Picha katika ukurasa wa 19]
Kuuawa kwa Dyuki Mkuu Ferdinand
[Hisani]
© Mary Evans Picture Library
-