-
Kufisha Babuloni MkubwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na pembe kumi ambazo wewe uliona humaanisha wafalme kumi, ambao bado kupokea ufalme, lakini wao hupokea mamlaka wakiwa wafalme saa moja pamoja na hayawani-mwitu.
-
-
Kufisha Babuloni MkubwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
12. (a) Pembe kumi ni picha ya nini? (b) Ni jinsi gani pembe kumi za ufananisho ‘hazikuwa zimepokea ufalme’? (c) Pembe kumi za ufananisho zinakuwaje na “ufalme” sasa, na ni kwa muda gani?
12 Pembe kumi ni picha ya serikali zote za kisiasa ambazo zinatawala sasa katika mandhari ya ulimwengu na ambazo huunga mkono hayawani-mwitu. Ni nchi chache sana zilizoko sasa ambazo zilijulikana katika siku ya Yohana. Na zile zilizojulikana, kama Misri na Uajemi (Irani), leo zina muundo wa kisiasa ulio tofauti kabisa. Kwa sababu hiyo, katika karne ya kwanza, ‘pembe kumi hazikuwa zimepokea ufalme.’ Lakini sasa katika siku ya Bwana, zina “ufalme,” au mamlaka ya kisiasa. Milki kubwa-kubwa za kikoloni zilipoanguka, hasa tangu vita ya ulimwengu ya pili, mataifa mengi mapya yamezaliwa. Hizi, pamoja na serikali ambazo zimeimarika muda mrefu, lazima zitawale pamoja na hayawani-mwitu kwa kipindi kifupi—“saa moja” tu—kabla Yehova hajakomesha mamlaka zote za kisiasa za ulimwengu kwenye Har–Magedoni.
-