Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ujumbe Mtamu na Mchungu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 2 “Na mimi nikaona malaika mwingine kabambe akishuka kutoka katika mbingu, akiwa amepambwa wingu, na upinde-mvua ulikuwa juu ya kichwa chake, na uso wake ulikuwa kama jua, na nyayo zake zilikuwa kama nguzo zenye moto.”—Ufunuo 10:1, NW.

  • Ujumbe Mtamu na Mchungu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Si uso pekee bali pia nyayo za malaika huyu ni zenye utukufu, “kama nguzo zenye moto.” Msimamo wake imara ni ule wa Mmoja ambaye Yehova amempa “mamlaka yote . . . katika mbingu na juu ya dunia.”—Mathayo 28:18; Ufunuo 1:14, 15, NW.

      5. Yohana anaona nini katika mkono wa malaika kabambe?

      5 Yohana huonelea zaidi: “Na katika mkono wake yeye alikuwa na hati-kunjo ndogo iliyofunguliwa. Na yeye akaweka wayo wake wa kulia juu ya bahari, lakini ule wa kushoto juu ya dunia.” (Ufunuo 10:2, NW)

  • Ujumbe Mtamu na Mchungu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 6. (a) Ni kwa nini inafaa kwamba nyayo za Yesu ziko juu ya bahari na dunia? (b) Zaburi 8:5-8 ilitimizwa kabisa kabisa wakati gani?

      6 Acheni turudi kwenye elezo kuhusu Yesu. Nyayo zake zenye moto ziko juu ya dunia na bahari, ambazo juu yazo yeye anatumia mamlaka kamili. Ni kama vile imetaarifiwa katika zaburi ya kiunabii: “Pia wewe [Yehova] uliendelea kumfanya yeye [Yesu] punde kidogo kuliko wafanana-mungu, kwa utukufu na umaridadi mno ndipo wewe ukavika yeye taji. Wewe ulifanya yeye amiliki juu ya kazi za mikono yako; kila kitu wewe umeweka chini ya nyayo zake: ng’ombe wadogo na maksai vyote hivyo, na pia hayawani wa konde lililo wazi, ndege wa mbingu na samaki wa bahari, kitu chochote kinachopita katika vijia vya zile bahari.” (Zaburi 8:5-8, NW; ona pia Waebrania 2:5-9.) Zaburi hii ilitimizwa kikamili katika 1914, wakati Yesu alipowekwa awe Mfalme wa Ufalme wa Mungu nao wakati wa mwisho ukaanza. Hivyo, yale anayoona Yohana hapa katika njozi yanahusu tangu mwaka huo.—Zaburi 110:1-6; Matendo 2:34-36; Danieli 12:4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki