Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ndege Ziliwasilije?
    Amkeni!—1999 | Machi 8
    • WABUNI walifanikiwaje mwishowe kutokeza mashine zinazoruka angani zilizo nzito kuliko hewa? Walielekeza uangalifu wao kwa wasanii stadi wa safari za angani—ndege wanaopuruka. Katika mwaka wa 1889 mhandisi Mjerumani aliyeitwa Otto Lilienthal, akichochewa na mazoea ya koikoi ya kusafiri angani, alichapisha kitabu “Bird Flight as the Basis of Aviation.” Miaka miwili baadaye alijenga nyiririko yake ya kwanza iliyo sahili. Katika mwaka wa 1896, baada ya safari za angani 2,000 za nyiririko, Lilienthal alikufa alipokuwa akifanyia majaribio ndege ya bawa moja. Octave Chanute, mhandisi Mmarekani aliyezaliwa Ufaransa, alifanyia marekebisho muundo wa Lilienthal na kutokeza nyiririko ya injini mbili ambayo nayo ilipiga hatua kubwa katika kuunda mashine inayoruka angani iliyo nzito kuliko hewa.

      Kisha akina Wright wakajitokeza. Orville na Wilbur Wright walikuwa na duka la baiskeli katika Dayton, Ohio, Marekani, nao walianza majaribio yao ya kwanza ya kunyiririka mwaka wa 1900, wakitegemea msingi uliowekwa na Lilienthal na Chanute. Akina Wright walifanya kazi polepole na kwa utaratibu kwa miaka mitatu iliyofuata, wakifunga safari za angani za majaribio mara kadhaa katika Kitty Hawk, North Carolina. Walitokeza miundo mipya inayotumia mashimo ya kupitishia upepo, na kwanza walitengeneza kwa kutumia sanduku la wanga. Katika safari yao ya kwanza ya angani kwa kutumia injini, walitengeneza injini yao wenyewe yenye silinda nne na nguvu-farasi 12 na kuipandisha kwenye bawa la chini la ndege mpya. Injini hiyo iliendesha rafadha mbili za mbao, moja katika kila upande wa usukani wa nyuma wa ndege.

      Mnamo Desemba 14, 1903, ndege mpya iliyovumbuliwa na akina Wright ilipaa kutoka kwenye ubao wa kuipeperushia kwa mara ya kwanza—na kubaki hewani kwa sekunde tatu u nusu! Siku tatu baadaye ndugu hao walipaa wakitumia mashine hiyo tena. Hatimaye ilibaki hewani kwa karibu dakika moja na kusafiri umbali wa meta 260. Ndege hiyo ikafanikiwa.a

      Kwa kushangaza, utimizo huo mkubwa haukuvutia uangalifu wowote wa ulimwengu. Hatimaye wakati The New York Times lilipochapisha habari kuhusu akina Wright katika Januari 1906, lilisema kwamba “mashine ya kuruka angani” ilikuwa imebuniwa kwa siri kubwa na kwamba ndugu hao walikuwa wamepata “mafanikio kidogo tu ya kusafiri angani” mwaka wa 1903. Kwa kweli, Orville alikuwa amempelekea baba yake telegramu usiku huohuo wa safari hiyo ya kihistoria, akimsihi aeleze vyombo vya habari. Hata hivyo, ni magazeti ya habari matatu tu huko Marekani yaliyojishughulisha kuchapisha habari hiyo wakati huo.

  • Ndege Ziliwasilije?
    Amkeni!—1999 | Machi 8
    • a Watu fulani wanadai kwamba mnamo mwaka wa 1901, Gustave Whitehead (Weisskopf), mhamiaji Mjerumani aliyeishi Connecticut, Marekani, pia aliendesha ndege aliyoibuni. Hata hivyo, hakuna picha za kuthibitisha dai hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki