-
Imani Yao Ilishinda Jaribu KaliSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
4. Fafanua roho ya kidini ya Babiloni.
4 Kwa kweli, mambo ya kidini yalienea kotekote Babiloni. Jiji hilo lilikuwa na mahekalu zaidi ya 50, ambamo miungu mingi ya kiume na ya kike iliabudiwa, kutia ndani ule utatu wa Anu (mungu wa anga), Enlil (mungu wa dunia, hewa, na dhoruba), na Ea (mungu aliyetawala maji). Utatu mwingine ulikuwa wa Sin (mungu-mwezi), Shamash (mungu-jua), na Ishtar (mungu wa kike wa uwezo wa kuzaa). Mizungu, uchawi, na unajimu zilitumiwa sana katika ibada ya Babiloni.
-
-
Imani Yao Ilishinda Jaribu KaliSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
1. Mnara wa hekalu (“ziggurat”) huko Babiloni
2. Hekalu la Marduki
-