-
Biblia—Kitabu cha Unabii Sahihi, Sehemu ya 2Amkeni!—2012 | Juni
-
-
Bamba moja gumu linalojulikana kama Mwanzi wa Koreshi, linakadiriwa kuwa la mwaka wa 539 K.W.K. hivi, mwaka uleule ambao Mfalme Koreshi wa Uajemi aliipindua Milki ya Babiloni. Sehemu fulani ya maandishi hayo inasema hivi: “Mimi ni Koreshi, . . . mfalme wa Babiloni.” Maandishi hayo yanaendelea kusema hivi: “Nilirudisha kwenye majiji matakatifu [ambayo tayari yalikuwa yametajwa] yaliyokuwa upande ule mwingine wa Tigri, majengo matakatifu ambayo yamekuwa magofu kwa muda mrefu sana, [na] sanamu zilizokuwepo ndani yake . . . Mimi (pia) niliwakusanya wakazi wake wote (wa awali) na nikawarudishia makao yao.”
Maandishi hayo yanapatana na unabii wa Biblia unaosema kwamba Wayahudi waliohamishwa wangerudishwa nyumbani kwao—unabii uliokuwa umerekodiwa miaka 200 hivi mapema.
-
-
Biblia—Kitabu cha Unabii Sahihi, Sehemu ya 2Amkeni!—2012 | Juni
-
-
[Picha katika ukurasa wa 13]
Maandishi kwenye Mwanzi wa Koreshi yanaonyesha sera ya Koreshi ya kuwarudisha mateka nyumbani kwao
-