-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 4Amkeni!—2011 | Februari
-
-
Historia Inayotegemeka
Biblia inatuambia kwamba Mfalme Koreshi wa Pili aliwaachilia huru Wayahudi waliokuwa mateka huko Babiloni, akawaruhusu kurudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu la Mungu ambalo Wababiloni waliharibu katika mwaka wa 607 K.W.K. (Ezra 1:1-7; 6:3-5) Simulizi hilo linaungwa mkono na maandishi yaliyoandikwa kwenye silinda ya udongo inayoitwa Cyrus Cylinder iliyopatikana kwenye magofu ya Babiloni la kale mwaka wa 1879. Maandishi hayo yanamtaja Koreshi kwa jina na kueleza sera yake ya kuwaruhusu mateka warudi nchini kwao pamoja na vyombo vyao vya kidini.
-
-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 4Amkeni!—2011 | Februari
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16, 17]
Silinda inayoitwa Cyrus Cylinder inaeleza sera ya kuwarudisha mateka nchini kwao
-