-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na huyo mwanamke alikuwa amepambwa zambarau na nyekundu-nyangavu na alikuwa amerembwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu na katika mkono wake alikuwa na kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake. Na juu ya kipaji cha uso wake paliandikwa jina, fumbo: ‘Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia.’
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Yeye ndiye “mama ya makahaba” kwa sababu dini bandia zote moja moja katika ulimwengu, kutia ndani mafarakano katika Jumuiya ya Wakristo, ni kama mabinti wake, zikimwiga yeye katika kufanya ukahaba wa kiroho.
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
25. (a) Ni nini kinachofananishwa na “kikombe cha dhahabu ambacho kilijaa vitu vya kunyarafisha?” (b) Ni katika maana gani kahaba wa ufananisho amelewa?
25 Tazama sasa alicho nacho kahaba huyu mkononi mwake. Haikosi Yohana alitweta kwa mshangao kukiona—kikombe cha dhahabu “kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake”! Hiki ndicho kikombe ambacho ndani yacho mna “divai ya kasirani ya uasherati wake” ambacho kwa hicho amefanya mataifa yote yalewe. (Ufunuo 14:8; 17:4) Kwa nje kinaonekana kuwa chenye utajiri, lakini yaliyomo ni yenye kunyarafisha, si safi. (Linga Mathayo 23:25, 26.) Ndani kina mazoea yote machafu na uwongo mwingi ambao huyo kahaba mkubwa ametumia kutongoza mataifa na kuwaleta chini ya uvutano wake.
-