Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Malaika anatuambia hapa kwamba “Babuloni Mkubwa . . . alifanya mataifa yote yanywe ya divai ya kasirani ya uasherati wake.” Hii humaanisha nini? Huhusiana na ushindi. Mathalani, Yehova alimwambia Yeremia: “Chukua kikombe hiki cha divai ya hasira-kali kutoka mkono wangu, na wewe lazima ufanye mataifa yote ambayo kwayo mimi ninatuma wewe yanywe hicho. Na wao lazima wanywe na kuyumbayumba na kutenda kama watu wenye kichaa kwa sababu ya upanga ambao mimi ninapeleka miongoni mwao.” (Yeremia 25:15, 16, NW) Katika karne ya sita na ya saba K.W.K, Yehova alitumia Babuloni ya kale kumwaga kikombe cha ufananisho cha dhiki kwa ajili ya mataifa mengi yanywe kutia na Yuda yenye kuasi imani, hivi kwamba hata watu wake mwenyewe walipelekwa katika uhamisho. Kisha, kwa zamu yayo, Babuloni ikaanguka kwa sababu ya mfalme wayo kujitukuza mwenyewe dhidi ya Yehova, “Bwana ya zile mbingu.”—Danieli 5:23, NW.

      5 Babuloni Mkubwa amefanya ushindi mwingi, lakini kwa sehemu iliyo kubwa, huo umekuwa wa werevu zaidi. Yeye ‘amefanya mataifa yote yanywe’ kwa kutumia ujanja wa kahaba, kufanya uasherati wa kidini pamoja nao. Yeye ametongoza watawala wa kisiasa waingie ndani ya mafungamano na urafiki pamoja naye. Kupitia vivuta-macho vya kidini, yeye amefanya njama ya uonevu wa kisiasa, wa kibiashara na wa kiuchumi. Yeye amechochea minyanyaso ya kidini na vita na krusedi, pamoja na vita vya kitaifa, kwa sababu tu za kisiasa na za kiuchumi. Naye ametakasa vita hivyo kwa kusema eti ni mapenzi ya Mungu.

      6 Kujiingiza kwa dini katika vita na siasa za karne ya 20 ni jambo linalojulikana na watu wote—kama katika Japani ya Shinto, India ya Hindu, Vietnamu ya Kibudha, Ailandi Kaskazini ya Ukristo” Amerika ya Kilatini, na nyinginezo—bila kusahau wale makasisi wa kijeshi pande zote mbili za vita viwili vya ulimwengu katika kuhimiza wanaume vijana wachinjane. Kielelezo kimoja bora cha kujiingiza kwa Babuloni Mkubwa ni hisa aliyokuwa nayo katika Vita ya Hispania ya Wenyewe kwa Wenyewe ya 1936-39, ambayo katika hiyo angalau watu 600,000 waliuawa. Umwagaji-damu huu ulichochewa na waungaji-mkono wa viongozi wa kidini Wakatoliki na wafungamani wao, kwa sehemu, kwa sababu ukwasi na cheo cha kanisa vilitishwa na serikali halali ya Hispania.

  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 208]

      ‘Divai ya Uasherati Wake’

      Sehemu Yenye Kutokeza ya Babuloni Mkubwa ni Kanisa Katoliki la Roma. Kanisa hilo linatawalwa na papa katika Roma nalo linadai kwamba kila papa ni mwandamizi wa mtume Petro. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya hakika yaliyochapishwa ya hawa wanaoitwa eti waandamizi:

      Formoso (891-96): “Miezi tisa baada ya kifo chake, mwili wa Formoso ulifukuliwa kutoka kaburi la mapapa na kushtakiwa ili kujaribiwa mbele ya baraza linalohukumu maiti, ambalo katika hilo Stefano [papa mpya] alisimamia. Huyo papa aliyekufa alishtakiwa kosa la kutaka makuu kupita kiasi kwa ajili ya cheo cha papa na matendo yake yote yalijulishwa wazi kuwa si halali. . . . Maiti hiyo ilivuliwa majoho ya kipapa; vidole vya mkono wa kulia vikakatwa.”—New Catholic Encyclopedia.

      Stefano 6 (896-97): “Kwa muda wa miezi michache [ya jaribio la maiti ya Formoso] tendo-mwitikio lenye jeuri lilikomesha upapa wa Papa Stefano; yeye alinyang’anywa nishani ya upapa, akatiwa gerezani, na akanyongwa.”—New Catholic Encyclopedia.

      Sergio 3 (904-11): “Watangulizi wake wawili wa karibu-karibu . . . walinyongwa gerezani. . . . Katika Roma yeye aliungwa mkono na jamaa ya Theofilakto, ambayo kwa mmoja wa mabinti yayo, Marozia, yeye anadhaniwa kuwa alikuwa amepata mwana (baadaye Papa John wa 11).”—New Catholic Encyclopedia.

      Stefano 7 (928-31): “Katika miaka ya mwisho ya upapa wake, Papa John 10 . . . amejiletea hasira-kisasi ya Marozia, aliyekuwa Donna Senatrix wa Roma, naye alikuwa ametiwa gerezani na kuuawa kwa hila. Ndipo Marozia akampa Papa Leo wa 6 upapa, ambaye alikufa miezi 6 1/2 katika ofisi. Stefano 7 akamwandamia, yaelekea kupitia uvutano wa Marozia. . . . Wakati wa miaka 2 yake akiwa Papa, yeye alikuwa hana nguvu chini ya utawala wa Marozia.”—New Catholic Encyclopedia.

      John 11 (931-35): “Stefano 7 alipokufa . . . , Marozia, wa Nyumba ya Theofilakto, alipata upapa kwa ajili ya mwanaye John, kijana katika miaka yake ya 20 na kitu. . . . Akiwa papa, John alitawalwa na mamaye.”—New Catholic Encyclopedia.

      John 12 (955-64): “Yeye alikuwa hajatimiza [miaka] kumi na minane, na ripoti za wakati wake hukubaliana juu ya kutopendezwa kwake na vitu vya kiroho, kuzoelea anasa zisizo za adabu, maisha ya ufasiki yasiyozuiliwa.”—The Oxford Dictionary of Popes.

      Benedikto 9 (1032-44; 1045; 1047-48): “Yeye alikuwa mwenye sifa mbaya ya kuuzia mdhamini wa ubatizo wake upapa na kisha kudai tena mara mbili cheo hicho baadaye.”—The New Encyclopædia Britannica.

      Hivyo, badala ya kufuata kielelezo cha Petro mwaminifu, hawa na mapapa wengine walikuwa uvutano mbovu. Wao waliachilia hatia ya damu na uasherati wa kiroho na wa kimwili, pamoja na uvutano wa Kiyezebeli, ufisidi kanisa walilotawala. (Yakobo 4:4) Katika 1917 kitabu The Finished Mystery cha Wanafunzi wa Biblia kilionyesha waziwazi sana kwa urefu mengi ya mambo haya ya hakika. Hii ilikuwa njia moja ambayo Wanafunzi wa Biblia katika siku hizo ‘walipiga dunia kwa kila aina ya tauni.’—Ufunuo 11:6; 14:8; 17:1, 2, 5, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki