Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na pembe kumi ambazo wewe uliona, na hayawani-mwitu, hizi zitachukia kahaba na zitafanya yeye kuwa mwenye kuteketezwa na mwenye uchi, na zitakula kabisa sehemu zake zenye mnofu na zitachoma yeye kabisa kabisa kwa moto.’”—Ufunuo 17:15, 16, NW.

      16. Ni kwa nini Babuloni Mkubwa hataweza kutegemea maji yake yamuunge mkono wa himaya wakati serikali za kisiasa zinapomgeukia?

      16 Kama vile Babuloni wa kale alivyotegemea ulinzi wa maji yake, Babuloni Mkubwa leo anategemea washiriki wake wengi mno “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi.” Kwa kufaa malaika huelekeza uangalifu wetu kwenye hao kabla ya kusimulia tukio lenye kugutusha: Serikali za kisiasa za dunia hii zitamgeukia kijeuri Babuloni Mkubwa.

  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 17. (a) Ni kwa sababu gani ukwasi wa Babuloni Mkubwa hautamwokoa? (b) Mwisho wa Babuloni Mkubwa utakuwaje wenye aibu kabisa? (c) Mbali na pembe kumi, au mataifa moja moja, ni nini kingine kinachojiunga katika jeuri dhidi ya Babuloni Mkubwa?

      17 Kwa hakika, ukwasi mkubwa mno wa vitu vya kimwili hautaweza kumwokoa Babuloni Mkubwa. Huenda hata ukaharakisha kuharibiwa kwake, kwa kuwa njozi huonyesha kwamba wakati hayawani-mwitu na pembe kumi wanapomwonyesha chuki yao watamvua majoho yake ya kifalme na vito vyake vyote vya thamani. Wao watapora ukwasi wake. ‘Wanamfanya kuwa uchi,’ wakifichua kiaibu tabia yake halisi. Mteketezo wee! Pia mwisho wake ni wenye aibu kabisa. Wanamharibu, na ‘kula sehemu zake zenye mnofu,’ wakimwacha mifupa mitupu isiyo na uhai. Mwishowe, wao ‘humchoma kabisa kabisa kwa moto.’ Yeye huchomwa kabisa kama mwenye ugonjwa wa tauni, bila hata maziko ya heshima!

  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika 607 K.W.K., Yehova alitumia Nebukadneza ‘avue mavazi, atwae vitu vizuri, na aache uchi na bila nguo’ jiji hilo lenye uzinzi wa kiroho. (Ezekieli 23:4, 26, 29, NW) Yerusalemu la wakati huo lilikuwa kigezo cha Jumuiya ya Wakristo ya leo, na kama alivyoona Yohana katika njozi ya mapema zaidi, Yehova ataipa Jumuiya ya Wakristo na dini nyingine yote bandia adhabu inayofanana na hiyo. Ukiwa, hali ya kutokaliwa ya Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. huonyesha vile Jumuiya ya Wakristo ya kidini itakavyoonekana baada ya kuvuliwa ukwasi wayo na kufichuliwa kiaibu. Na sehemu inayobaki ya Babuloni Mkubwa haitakuwa afadhali.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki