Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Estonia
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Katika miaka ya 1950, Fanny alitumika kama mjumbe na alibeba barua na mikanda ya filamu yenye maandishi madogo kutoka Finland hadi Estonia. Alikuwa mwenye ujasiri na busara, na ingawa nyakati nyingi hali zilikuwa zenye kufadhaisha, hakuwahi kukamatwa. Kwa mfano, wakati mmoja alisafiri hadi Leningrad (St. Petersburg) kuchukua kifurushi cha mikanda ya filamu kilichokuwa kimeletwa na ndugu wa Finland. Alikuwa akutane naye katika bustani fulani. Fanny naye, alipaswa kupitisha kifurushi hicho haraka iwezekanavyo kwa ndugu wawili Waestonia. Hata hivyo, ndugu hao Waestonia walikuwa wamegundua kwamba wanafuatwa na polisi wa siri na hivyo wakajaribu kuondoka bila Fanny kuwaona. Lakini wapi! Fanny na yule ndugu wa Finland walitembea moja kwa moja wakielekea mahali ndugu hao walipokuwa. Kama Fanny angewasalimu au kujaribu kuwapa kile kifurushi, polisi hao wa siri wangejua mipango yao. Kwa kushangaza, Fanny aliwapita ndugu hao kana kwamba hakuwajua. Baadaye, waligundua kwamba Fanny hakuwaona, ingawa aliwajua vizuri sana! Kwa hiyo, polisi hao wa siri hakuweza kuwatambua wajumbe hao na baadaye ndugu Waestonia waliweza kupata kile kifurushi. Akiwa mjumbe, Fanny aliwasaidia akina ndugu nchini Estonia kupata chakula cha kiroho kwa ukawaida, na hakuna mikanda yoyote ya filamu ambayo polisi waliipata.

  • Estonia
    2011 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha]

      Kusafirisha chakula cha kiroho jijini Leningrad, 1966

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki