Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hangaiko Langu Kuu—Kudumu Mwaminifu
    Amkeni!—2000 | Oktoba 8
    • Ulikuwa mwaka wa 1947; mahali palikuwa kilometa chache kutoka kijiji chetu cha Laskiv, Ukrainia, karibu na mpaka wa Poland. Stepan, rafiki yangu mwenye umri mkubwa kuliko mimi, alitumikia kama mjumbe aliyepeleka kwa siri vichapo vya Biblia Ukrainia kutoka Poland. Usiku mmoja mlinzi wa mpakani alimwona, akamfuata, akampiga risasi. Miaka 12 baadaye kifo cha Stepan kiliathiri sana maisha yangu, kama nitakavyoeleza baadaye.

  • Hangaiko Langu Kuu—Kudumu Mwaminifu
    Amkeni!—2000 | Oktoba 8
    • Kufanya Kazi Kisiri

      Wasovieti walirudi Ukrainia mwezi wa Agosti 1944, na Vita ya Ulimwengu ya Pili ilikoma huko Ulaya mwezi wa Mei 1945. Baadaye, sisi tulioishi Muungano wa Sovieti tulitengwa na sehemu nyingine za ulimwengu na kile kilichoitwa Pazia la Chuma. Hata ilikuwa vigumu kuwasiliana na Mashahidi wa Yehova waliokuwa upande mwingine wa mpaka huko Poland. Mashahidi wajasiri walivuka mpaka na kurudi na nakala chache zenye thamani za gazeti la Mnara wa Mlinzi. Kwa kuwa mpaka ulikuwa umbali wa kilometa nane tu kutoka nyumbani kwetu Laskiv, nilisikia kuhusu hatari ambazo wajumbe hao walipitia.

      Kwa mfano, Shahidi mmoja aitwaye Silvester alivuka mpaka mara mbili na kurudi bila matatizo. Lakini safari ya tatu walinzi wa mpakani na mbwa wao walimwona. Wanajeshi hao walimpaazia sauti asimame, lakini Silvester alikimbia kuokoa uhai wake. Hakuwa na njia nyingine kuepuka mbwa hao isipokuwa kuingia katika ziwa lililokuwa karibu. Alikaa usiku kucha katika maji yaliyomfika shingoni, akijificha katikati ya nyasi ndefu. Hatimaye, walinzi walipoacha kumtafuta, Silvester alirudi nyumbani, akiwa amechoka kabisa.

      Kama ilivyotajwa mwanzoni, mpwa wa Silvester, Stepan, aliuawa alipojaribu kuvuka mpaka huo. Hata hivyo, kuwasiliana na watu wa Yehova kulikuwa jambo muhimu. Kupitia jitihada za wajumbe wajasiri, tuliweza kupokea chakula cha kiroho na maagizo yaliyotusaidia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki