Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwaka wa 1944, majeshi ya Ujerumani yaliondoka Albania, na majeshi ya Kikomunisti yakaanzisha serikali ya mpito. Mara moja, akina ndugu wakatuma maombi ya kuchapisha upya vijitabu, lakini ombi lao halikukubaliwa. “Mnara wa Mlinzi linashambulia makasisi,” ndugu wakaambiwa, “nasi hapa Albania bado tunawaheshimu makasisi.”

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Serikali ilitunyang’anya vitabu, karatasi chache zilizokuwa zimebaki, na taipureta kadhaa ambazo akina ndugu walikuwa nazo.

      Kila mara akina ndugu walipojaribu kuomba kibali cha kuchapisha vitabu, walinyimwa na kutishwa. Hata hivyo, walisimama imara. “Yehova ametupa jukumu la kuwajulisha watu wa Albania makusudi yake,” wakawaambia wenye mamlaka, “nanyi mnatuzuia. Shauri yenu.”

      Ni kana kwamba wenye mamlaka walisema: ‘Hapa Albania sisi ndio wenyewe! Serikali yetu si ya kitheokrasia, nasi hatuna haja nanyi wala Mungu wenu, Yehova, ambaye hata hatumtambui!’ Ndugu hao hawakukata tamaa bali waliendelea kuhubiri habari njema mahali popote na wakati wowote ambapo wangeweza.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki