-
TulishirikianaMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
Kazi Yetu Yapigwa Marufuku
Jumamosi, Januari 18, 1941, wenye mamlaka katika serikali walikuja kwenye ofisi ya tawi kwa magari sita hivi meusi ili kunyakua ofisi hiyo. Kwa kuwa nilikuwa nikifanya kazi katika nyumba ndogo ya kupokelea wageni kwenye lango la Betheli, mimi ndiye niliyewaona kwanza. Muda wa saa 18 awali, tulikuwa tumearifiwa kuhusu marufuku hayo, kwa hiyo karibu vichapo vyote na faili zilikuwa zimeondolewa kwenye ofisi ya tawi. Juma lililofuata, washiriki watano wa familia ya Betheli, pamoja na Lloyd, walitiwa gerezani.
-
-
TulishirikianaMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
Mnamo Mei 1942, familia ya Betheli ilikuwa imehama ofisi ya Strathfield na kwenda katika nyumba za watu binafsi. Walihama kutoka nyumba moja hadi nyingine kila baada ya majuma kadhaa ili wasigunduliwe. Wakati mimi na Lloyd tuliporudi Betheli mwezi wa Agosti, tulijiunga na familia hiyo katika mojawapo ya nyumba hizo. Mgawo wetu mchana ulikuwa kufanya kazi kwenye mojawapo ya matbaa iliyokuwa imeanzishwa kisiri. Hatimaye, mnamo Juni 1943, marufuku dhidi ya kazi yetu yakaondolewa.
-