-
“Jinsi Inavyotamanika Imani Isiyofifia”!Mnara wa Mlinzi—2000 | Novemba 1
-
-
Hata ingawa chakula kilikuwa haba, Erika hakukosa kamwe chakula kwa jamaa. (Mathayo 6:33) Mkulima Mkatoliki, ambaye nilikuwa nimemrekebishia cherehani alimpa viazi. Pia alimpasha Erika habari kutoka kwangu. Wakati mmoja, Erika alilipa guldeni moja kwa kitu alichonunua katika duka la dawa. Mwenye duka aliyejua anaishi mafichoni na hangeweza kupata kadi ya posho, alimpa kile alichotaka kununua na pia guldeni mbili. Vitendo vya huruma vya namna hiyo vilimsaidia kuendelea kuishi.—Waebrania 13:5.
-
-
“Jinsi Inavyotamanika Imani Isiyofifia”!Mnara wa Mlinzi—2000 | Novemba 1
-
-
Zaidi ya hayo, tulipanga kusafirisha chakula kutoka katika mashamba yaliyokuwa mashariki ya Uholanzi hadi majiji ya magharibi, ijapokuwa jambo hilo lilikatazwa. Tukapakia chakula kwenye gari lililovutwa na farasi na kuelekea magharibi. Tulipofika mtoni, hatukuweza kuvuka kwa kutumia madaraja yoyote kwa kuwa yalilindwa na wanajeshi. Badala yake, tulihamisha mizigo kwenye mashua ndogo, mashua hizo zikavuka mto mara kadhaa zikiwa na chakula, halafu tukapakia mizigo kwenye gari jingine la farasi. Tulipofika jiji la mwisho wa safari yetu, tulingoja hadi usiku, tukavisha farasi soksi kwenye kwato, na bila kufanya kelele tukaelekea mahali pa kutaniko pa kuficha chakula. Hapo chakula kiligawanywa na kupelekwa kwa akina ndugu wenye uhitaji.
Ikiwa jeshi la Ujerumani lingaligundua mahali kama hapo pa kuficha chakula, ingaliweza kusababisha mtu auawe. Hata hivyo, ndugu kadhaa walijitoa kusaidia kufanya kazi hiyo. Kwa mfano jamaa ya Bloemink katika mji wa Amersfoort, walitoa sebule yao itumiwe kama ghala ya chakula, ijapokuwa nyumba yao ilikuwa karibu sana na ngome ya jeshi la Ujerumani! Mashahidi wajasiri kama hao walihatarisha uhai wao kwa ajili ya ndugu zao.
-