Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Baba Asiye na Kifani
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Januari 1
    • Tazama! Kulikuwa pia na sauti kutoka mbinguni iliyosema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ambaye nimemkubali.’”a (Mathayo 3:16, 17) Maneno hayo mororo yaliyosemwa na Yehova mwenyewe yanatuambia mengi kuhusu Yeye ni Baba wa aina gani. Ona mambo matatu ambayo Yehova alimwambia Mwana wake.

      Kwanza, kwa kusema “huyu ni Mwanangu,” kwa kweli, Yehova alikuwa akisema, ‘Ninajivunia kuwa Baba yako.’ Baba mwenye utambuzi anatosheleza tamaa ya watoto wake ya kuthaminiwa na kupewa uangalifu. Watoto wanahitaji kuhakikishiwa kwamba wanathaminiwa wakiwa washiriki muhimu wa familia. Wazia jinsi Yesu alivyohisi Baba yake alipomhakikishia kwamba anamthamini, hata ingawa alikuwa mtu mzima!

      Pili, kwa kumwita Mwana wake, “mpendwa,” Yehova alionyesha waziwazi kwamba anampenda Yesu. Kwa maneno mengine, Baba alikuwa akisema, ‘Ninakupenda.’ Baba mzuri anawaambia watoto wake kwamba anawapenda sana. Maneno kama hayo yanapoambatana na upendo wa kweli, yanawasaidia watoto kusitawi. Yesu aliguswa moyo kama nini kumsikia Baba yake akisema kwamba anampenda!

  • Baba Asiye na Kifani
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Januari 1
    • a Kulingana na simulizi la Injili ya Luka, Yehova alitumia neno “wewe,” aliposema: “Wewe ni Mwanangu, mpendwa; nimekukubali wewe.”—Luka 3:22.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki