Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Viumbe Wana Hisi za Ajabu
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • Wazia ukiwa na uwezo wa kusikia mdudu akitembea! Popo—mnyama pekee anayeweza kuruka kama ndege—ana uwezo huo. Bila shaka, popo wanahitaji uwezo wa kipekee wa kusikia ili kusafiri gizani na kukamata wadudu kwa kusikiliza mwangwi wa sauti yao wenyewe.e Profesa Hughes anasema hivi: “Hebu wazia mfumo wa kupokea mwangwi ulio tata kuliko ule wa nyambizi ya hali ya juu zaidi. Sasa wazia mfumo huo ukitumiwa na popo mdogo sana anayeweza kutoshea katika kiganja cha mkono wako. Ubongo wake ambao ni mdogo kuliko ukucha wa kidole gumba humwezesha kutambua umbali, mwendo, na hata aina ya wadudu anaonuia kukamata!”

      Ili popo watambue mahali vitu vilipo kwa usahihi, wanahitaji kutoa sauti nzuri. Wao hufanya hivyo kwa kutumia “uwezo wao wa ajabu wa kuinua na kushusha sauti ambao unapita ule wa mwimbaji bora,” chasema kitabu kimoja.f Inaonekana jamii fulani ya popo hutumia viungo fulani vilivyo juu ya pua zao kuelekeza sauti mahali fulani. Kwa kutumia uwezo huo, popo wanaweza kutambua hata vitu vidogo sana kama unywele wa mwanadamu!

  • Viumbe Wana Hisi za Ajabu
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • e Kuna aina 1,000 hivi za popo. Tofauti na maoni ya watu wengi, popo wote wanaweza kuona vizuri, lakini si wote wanaoweza kutumia mwangwi wa sauti zao. Baadhi yao, kama wale popo wanaokula matunda, hutumia uwezo wao wa kuona vizuri gizani kupata chakula.

      f Popo hutoa mlio wenye frikwensi tofauti-tofauti kuanzia hezi 20,000 hadi hezi 120,000 au zaidi.

  • Viumbe Wana Hisi za Ajabu
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 9]

      Enyi Wadudu, Jihadharini!

      “Kila siku, wakati wa jioni, jambo la kushangaza sana hutukia chini ya vilima vilivyo karibu na San Antonio, Texas [Marekani],” chasema kitabu Sensory Exotica—A World Beyond Human Experience. “Ukiwa mbali, unaweza kufikiri umeona wingu kubwa la moshi mweusi likipaa kutoka chini ya ardhi. Hata hivyo, si moshi unaofanya anga kuwa jeusi, bali ni popo milioni 20 wenye mikia mirefu ambao wanatoka katika Pango la Bracken.”

      Makadirio yaliyofanywa hivi karibuni yanaonyesha kwamba kuna popo milioni 60 katika Pango la Bracken. Popo hao hupaa kufikia meta 3,000 angani ili kutafuta wadudu, kwani hicho ndicho chakula wanachokipenda sana. Ijapokuwa sauti nyingi sana za popo zinasambaa angani wakati wa usiku, hakuna mvurugo wowote unaotokea kwani kila mmoja wa popo hao ana mfumo tata sana unaomsaidia kutambua mwangwi wake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki