-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
3. (a) Ni hayawani gani wakali sana alioona nabii Danieli katika njozi? (b) Hayawani wakubwa mno wa Danieli 7 waliwakilisha nini?
3 Huyu hayawani wa kiajabu ni nini? Biblia yenyewe hutoa jibu. Kabla ya anguko la Babuloni katika 539 K.W.K., Danieli nabii Myahudi aliona njozi zilizohusu hayawani wakali sana. Kwenye Danieli 7:2-8, NW yeye anaeleza habari za hayawani wanne wakitoka baharini, wa kwanza akishabihi simba, wa pili dubu, wa tatu chui, na “ona kule! hayawani wa nne, mwenye kuhofisha na mwenye kutisha na mwenye nguvu isivyo kawaida . . . na alikuwa na pembe kumi.” Huyu ni sawa kabisa na hayawani aliyeonwa na Yohana wapata mwaka 96 W.K. Pia hayawani huyo ana hulka za simba, dubu, na chui, na ana pembe kumi. Ni nini ulio utambulisho wa wale hayawani wakubwa mno walioonwa na Danieli? Yeye anatuarifu: “Hayawani hawa wakubwa mno . . . ni wafalme wanne ambao watasimama katika dunia.” (Danieli 7:17, NW) Ndiyo, hayawani hao wanawakilisha “wafalme,” au serikali kubwa za kisiasa za dunia.
4. (a) Katika Danieli 8, kondoo-dume na mbuzi-dume ni taswira ya nini? (b) Ni nini kilichoonyeshwa wakati upembe mkubwa wa mbuzi-dume ulipovunjwa na nyingine nne zikachukua mahali pao?
4 Katika njozi nyingine, Danieli anaona kondoo-dume mwenye pembe mbili ambaye anapigwa mpaka chini na mbuzi mwenye upembe mkubwa. Malaika Gabrieli anamweleza maana yayo: “Kondoo-dume . . . husimama kwa ajili ya wafalme wa Umedi na Uajemi. Na mbuzi-dume mwenye manyoya anasimama kwa ajili ya mfalme wa Ugiriki.” Gabrieli anaendelea kutoa unabii kwamba upembe mkubwa wa mbuzi-dume ungevunjwa na kufuatwa na pembe nne. Kwa kweli hilo lilitukia miaka zaidi ya 200 baadaye Aleksanda Mkuu alipokufa na ufalme wake ukagawanywa kuwa falme nne zilizotawalwa na wanne wa majenerali wake.—Danieli 8:3-8, 20-25, NW.a
5. (a) Neno la Kigiriki kwa hayawani linawasilisha maana gani? (b) Hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1, 2, pamoja na vichwa vyake saba anasimamia nini?
5 Kwa hiyo, ni wazi kwamba Mtungaji Biblia iliyovuviwa huziona serikali za kisiasa za dunia kuwa hayawani. Ni hayawani wa aina gani? Mfasili mmoja anaita hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1, 2 “mshenzi,” na kuongeza: “Sisi tunakubali maana zote ambazo θηρίον [the·riʹon, neno la Kigiriki kwa “hayawani”] huwasilisha, kama dubwana mkatili, mharibifu, mwenye kutia kikuli, mlafuaji, n.k.”b Lo! jinsi hiyo inavyoeleza vizuri mfumo wa kisiasa wenye madoa ya damu ambao kwa huo Shetani ametawala aina ya binadamu!
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8. Ni kwa nini haipasi kushtusha kwa vile Uingereza-Amerika serikali kubwa ya uwili, inafananishwa na hayawani?
8 Lakini je! haishtushi kutambulisha serikali za kisiasa na hayawani-mwitu? Ndivyo baadhi ya wapinzani walivyodai wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, hadhi ya Mashahidi wa Yehova, wakiwa tengenezo na wakiwa watu mmoja mmoja, ilipokuwa ikitiliwa shaka katika mahakama za sheria kotekote duniani. Lakini tua ufikirie! Je! mataifa yenyewe hayatumii hayawani au viumbe-mwitu kuwa ishara za kitaifa zao? Mathalani, kuna simba wa Uingereza, tai wa Amerika, na drakoni wa Uchina. Basi sababu gani yeyote apinge ikiwa Mtungaji wa kimungu wa Biblia Takatifu anatumia pia hayawani kufananisha serikali za ulimwengu?
-