Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na yeye [malaika] akapeleka mimi mbali kwa nguvu ya roho kuingia ndani ya jangwa. Na mimi nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye alikuwa amejaa majina ya kufuru na ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”—Ufunuo 17:3, NW.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 17. (a) Ni katika njia gani huyo hayawani-mwitu wa ufananisho rangi-nyekundu-nyangavu anajaa majina ya kufuru? (b) Ni nani anayempanda huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu? (c) Dini ya Kibabuloni ilijifungamanishaje na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao pale pale mwanzoni?

      17 Ni katika njia gani huyu hayawani-mwitu wa ufananisho anajaa majina ya kufuru? Katika njia ya kwamba wanadamu wameisimamisha sanamu hii ya kuabudiwa na mataifa mengi ikiwa kibadala cha Ufalme wa Mungu—itimize jambo ambalo Mungu husema ni Ufalme wake pekee unaoweza kutimiza. (Danieli 2:44; Mathayo 12:18, 21) Ingawa hivyo, jambo lenye kutokeza kuhusu njozi ya Yohana ni kwamba, Babuloni Mkubwa anapanda hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu. Kupatana na ukweli wa unabii, dini ya Kibabuloni, hasa katika Jumuiya ya Wakristo, imejifungamanisha yenyewe na Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao. Mapema kama Desemba 18, 1918, shirika ambalo sasa linajulikana kuwa Baraza la Taifa la Makanisa ya Kristo katika Amerika lilipitisha julisho-wazi lililojulisha wazi kwa sehemu hivi: “Ushirika kama huo si manufaa ya kisiasa tu; badala ya hivyo ni wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani. . . . Kanisa linaweza kutoa roho ya nia njema, ambayo bila hiyo hakuna Ushirika wa Mataifa unaoweza kudumu. . . . Ushirika wa Mataifa una mizizi katika Gospeli. Kama Gospeli, lengo lao ni ‘amani duniani, nia njema kuelekea wanadamu.’”

      18. Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walionyeshaje uungaji-mkono wao kwa Ushirika wa Mataifa?

      18 Katika Januari 2, 1919, San Fransisco Chronicle lilikuwa na kichwa kikuu cha habari kwenye ukurasa wa kwanza: “Papa Asihi Ukubaliwe Ushirika wa Maitafa wa Wilson.” Katika Oktoba 16, 1919, ombi rasmi lililotiwa sahihi na makasisi wa vikundi mashuhuri 14,450 lilitolewa kwenye Seneti ya U.S., kuhimiza baraza hilo ‘liidhinishe mwafaka wa amani wa Paris uliotia ndani agano la ushirika wa mataifa.’ Ingawa Seneti ya U.S. ilishindwa kuidhinisha mwafaka huo, viongozi wa Jumuiya ya Wakristo waliendelea kufanya kampeni kwa ajili ya huo Ushirika. Na Ushirika huo ulizinduliwaje? Habari iliyopelekwa kutoka Uswisi, yenye tarehe ya Novemba 15, 1920, ilisomwa hivi: “Kufunguliwa kwa kusanyiko la kwanza la Ushirika wa Mataifa kulitangazwa kwenye saa tano asubuhi hii kwa kupigwa kengele zote za kanisa katika Geneva.”

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 20. Ni kwa sababu gani ilikuwa kufuru viongozi wa kidini kushangilia Ushirika wa Mataifa kuwa “wonyesho wa kisiasa wa Ufalme wa Mungu duniani”?

      20 Ushinde wenye kusikitisha sana wa Ushirika wa Mataifa ulipaswa kuashiria viongozi wa kidini kwamba vyombo hivyo vyenye kufanywa na mwanadamu si sehemu ya Ufalme wa Mungu duniani. Ni kufuru kama nini kudai hivyo! Hufanya ionekane kana kwamba Mungu alishiriki kufanyiza Ushirika wa Mataifa ambao ni kazi ya ovyo sana. Kwa habari ya Mungu “utendaji wake ni mkamilifu.” Ufalme wa Yehova wa kimbingu chini ya Kristo—wala si muungano wa wanasiasa wenye kuzozana, wengi wao wakiwa hawaitikadi kuwako kwa Mungu—ndiyo njia ambayo kwayo yeye ataleta amani na kufanya penzi lake lifanywe duniani kama katika mbingu.—Kumbukumbu 32:4; Mathayo 6:10, NW.

      21. Ni nini kinachoonyesha kwamba kahaba mkubwa anaunga mkono na kusifu mno mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa?

      21 Namna gani mwandamizi wa Ushirika, Umoja wa Mataifa? Tangu mwanzo wao, baraza hili limekuwa na kahaba akilipanda mgongoni mwalo, akishirikiana nalo waziwazi na akijaribu kuongoza liendako. Mathalani, katika ukumbusho wa mwaka wao wa 20 katika Juni 1965, wawakilishi wa Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa Orthodoksi la Mashariki, pamoja na Waprotestanti, Wayahudi, Wahindu, Wabuddha, na Waislamu—waliosemekana kuwakilisha idadi ya watu wa dunia elfu mbili milioni—walikusanyika katika San Francisco kusherehekea uungaji-mkono na usifaji wao wa UM. Alipozuru UM Oktoba 1965, Papa Paul 6 alieleza habari zao kuwa “hilo tengenezo la kimataifa kubwa zaidi ya yote” na akaongeza: “Vikundi vya watu wa dunia vinategemea Umoja wa Mataifa kuwa ndilo tumaini la mwisho la itifaki na amani.” Mgeni mwingine wa kipapa, Papa John Paul 2, akihutubia UM katika Oktoba 1979, alisema: “Mimi natumaini Umoja wa Mataifa utadumu daima ukiwa ndilo baraza kuu la amani na haki.” Kwa uwazi sana, huyo papa alimtaja Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu mara chache sana katika hotuba yake. Wakati wa ziara yake United States katika Septemba 1987, kama ilivyoripotiwa na The New York Times, “John Paul alisema kirefu juu ya daraka chanya la Umoja wa Mataifa katika kuendeleza . . . ‘ushirikiano mpya wa ulimwenguni pote.’”

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 244]

      “Majina ya Kufuru”

      Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’

      “Ukristo unaweza kuandaa nia njema, nguvu-msukumo inayotendesha ushrika [wa mataifa], na hivyo kugeuza mwafaka huo kutoka kipande cha karatasi tu na kuwa chombo cha ufalme wa Mungu.”—The Christian Century, U.S.A., Juni 19, 1919, ukurasa 15.

      “Wazo la Ushirika wa Mataifa ni mpanuo kuelekea mahusiano ya kimataifa wa wazo la Ufalme wa Mungu ukiwa utaratibu wa ulimwengu wa nia njema. . . . Ndicho kitu ambacho Wakristo wote husali kwa ajili yacho wanaposema, ‘Ufalme wako uje.”—The Christian Century, U.S.A., Septemba 25, 1919, ukurasa 7.

      “Saruji ya Ushirika wa Mataifa ni Damu ya Kristo.”—Dakt. Frank Crane, Mhudumu Mprotestanti, U.S.A.

      Baraza [la Taifa la Makanisa ya Kongrigeshonali] huunga mkono Agano [la Ushirika wa Mataifa] kuwa ndicho chombo pekee cha kisiasa kinachopatikana sasa ambacho kwacho Roho ya Yesu Kristo inaweza kupata mweneo mpana zaidi katika utumizi wenye mafaa kwenye mambo ya mataifa.”—The Congregationalist and Advance, U.S.A., Novemba 6, 1919, ukurasa 642.

      “Kongamano lataka Wamethodisti wote wategemeze na kuendeleza sana mawazo bora [ya Ushirika wa Mataifa] kama yanavyoonyeshwa na wazo la Mungu Baba na watoto wa Mungu wa kidunia.”—Kanisa la Kimethodisti la Wesley, Uingereza.

      “Tunapoyafikiria malengo yale, mawezekano na maazimio ya mwafaka huu, sisi tunaona kwamba una moyo wa mafundisho ya Yesu Kristo: Ufalme wa Mungu na uadilifu wake . . . Si kitu kilicho punde ya huo.”—Mahubiri ya Askofu Mkuu wa Kantabari wakati wa kufunguliwa kwa Kusanyiko la Ushirika wa Mataifa katika Geneva, Desemba 3, 1922.

      “Shirika la ule Ushirika wa Mataifa katika nchi hii lina haki takatifu ile ile kama sosaiti ya kimisheni yoyote ya ufadhili-binadamu, kwa sababu kwa wakati uliopo ndicho chombo chenye matokeo zaidi sana cha utawala wa Kristo Mwana-Mfalme wa amani miongoni mwa mataifa.”—Dakt. Garvie, mhudumu Mkongrigeshonali, Uingereza.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki